TANZANIA-DIPLOMASIA

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania azituhumu nchi za ukanda wa maziwa makuu kuchochea machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benrad Membe
waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Benrad Membe

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Tanzania, Bernard Camilius Membe amesema kuwa mzozo unaoshuhudiwa mashariki mwa nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC unachangiwa na nchi wanachama za ukanda wa maziwa makuu.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na mwandishi wetu wa idhaa ya rfikingereza pembezoni mwa mkutano wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU, waziri Membe anakiri kuwa kwa sehemu kubwa mzozo wa mashariki ya kongo unachochewa na zenyewe zinazoizunguka nchi ya DRC na kwamba ni wao wenyewe ndio wanaoweza kumaliza ama kuendeleza machafuko.

Tulipomuuliza iwapo anataarifa za kuchapishwa kwa ripoti ya Umoja wa Mataifa inayozitaja nchi za rwanda na Uganda kuhusika na kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa M23, waziri Membe anasema hana taarifa hizo lakini anasisitiza kuwa jambo la muhimu ni kuyashirikisha makundi hayo kwenye mazungumzo ya kisiasa.

Katika hatua nyingine mkuu wa tume ya umoja wa mataifa nchini DRC, MONUSCO, Martin Kobler amesema kuwa kuanzia mwezi ujao wanatarajia kuongeza ndege zisizo na rubani kufanya doria kwenye mpaka wa Rwanda na Uganda na nchi ya DRC.