SUDANI-SUDAN KUSINI-Uchunguzi

Amnesty International yaomba uchunguzi uanzishwe nchini Sudan Kusini kuhusu mauwaji yanayoendelea

Raia waliyoyahama makaazi yao kufuatia mapigano chini Sudan Kusini
Raia waliyoyahama makaazi yao kufuatia mapigano chini Sudan Kusini RFI

hirika la Kimataifa la kutetea haki za Binadamu la Amnesty International linataka uchunguzi wa kikamilifu kufanyika nchini Sudan Kusini kubaini kuhusu mauaji ya maelfu ya watu na makosa mengine ya ukiukwaji wa haki za binadamu yanayotokea. Shirika hilo linasisitiza kuwa uchunguzi huo utasaidia waliochchea mauaji hayo kuajibishwa na kuanza kwa haraka juhudi za mariadhiano ya kitaifa.

Matangazo ya kibiashara

Askofu mkuu wa Kanisa la Anglikana katika jimbo la Cantebury nchni Uingreza Justin Welby yupo jijini Juba katika jitihada za kuhubiri amani katika taifa hilo.

Serikali ya Sudan Kusini na upinzani walitia saini mikataba miwili alhamisi januari 23 mwaka huu katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Mkataba  wa kwanza ni sitisho la haraka la hatua za kijeshi na wa pili unahusu kuachiliwa kwa wafungwa 11 wa kisiasa ambao wametiwa ndani tangu kuanza kwa mzozo katikati ya mwezi Disemba mwaka uliopita.

Hata hivyo hivi karibuni utawala wa Juba umewachia huru wanasiasa saba kati ya kumi na moja waliyokua wakishikiliwa , ambao wamekua wakidaiwa kuachiliwa huru na waasi wanao muunga mkono Riek Machar.

Awali Riek Machar alifahamisha kwamba haikua nia yao ya kuanzisha vita, bali walilazimishwa kufanya hivo.

Nchi ya Sudan Kusini inakabiliwa na mapigano toka tarehe 15 mwezi disemba, mapigano ambayo yanachochewa kutokana na malumbano kati ya rais Salva Kiir na aliekua makamo wake, ariek Machar.

Mapigano hayo yamesababisha mamia ya watu kupoteza maisha.