SYRIA

Marekani hayofia utekelezwaji wa kuondolewa kwa silaha za kemikali nchini Syria

Marekani inasema ni asilimia 4 tu ya silaha za kemikali zilizoondolewa nchini Syria hadi sasa kwa mujibu wa mkataba wa Umoja wa Mataifa. Waziri wa Ulinzi wa Marekani Chuck Hagel amesema hii inaamisha kuwa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuondoa silaha zote unacheleweshwa na kusisitiza kuwa ni sharti serikali ya Damascus iwajibike na kuharakisha zoezi hilo.

Matangazo ya kibiashara

Hagel ameitaka Urusi kuingilia kati suala hili na kusisitiza kuwa Marekani haielewi  na inahofu ni kwanini Syria haijatekeleza mpango huo wa Umoja wa Mataufa kuhusu silaha zake za kemikali ili ziharibiwe kwa wakati uliopangwa .

Wakati hayo yajikiri, wajumbe wa serikali na upinzani wanatarajiwa kutamatisha mzunguko wa pili wa mazungumzo ya amani leo Ijumaa jijini Geneva nchini Uswizi.

Msuluhishi wa Kimataifa wa  mgogoro huo Lakdhar Brahimi amesema kuwa hakuna mwafaka wowote utakaoafikiwa katika mazugumzo haya hasa kuhusu mjadala wa uundwaji wa serkali ya mpito wakati mazungumzo hayo yanapotamatishwa.

Hata hivyo, amesema kuwa ana matumaini mazungumzo hayo yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo yataanza kuzaa matunda ili kwa lengo la kupata amani ya kudumu nchini Syria.

Siku ya Alhamisi, wajumbe kutoka upande wa serikali na upinzani walitumia dakika moja wakiwa kimya  kuwakumbuka maelfu ya watu waliopoteza maisha nchini Syria huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon akisema atatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo yanazaa matunda katika siku zijazo.

Brahimi kwa upande mwingine, amedokeza kuwa amesikitishwa mno na kutotekelezwa kwa mwafaka uliofikiwa mapema juma hili kuwa raia wakubaliwe kuondoka katika mji wa Hoams na misaada ya kibinadamu kuruhusiwa kuwafikia.

Marekani inasema maelfu ya watu wanaishi katika mazingira magumu katika mji wa Homs,na wanakabiliwa na baa la njaa katika  mji ambao wanajeshi wa serikali wamekuwa wakiudhibiti kwa miezi kumi na minane sasa.