UKRAINE-Maandamano

Serikali ya Ukraine yaahidi kupatia ufumbuzi mgogoro unaoendelea

Polisi nchini Ukraine wakijihami kuzuia maandamano
Polisi nchini Ukraine wakijihami kuzuia maandamano RFI

Rais wa Ukraine Viktor Yanukovych amesisitiza kuwa yeye na serikali yake wanafanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kusuluhisha mgogogro unaoendelea nchini humo. Kauli ya rais Yanukovych inakuja baada ya kutangaza kuwa amekwenda kupumzika kwa sababu anaumwa. 

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji jijini Kiev wanasema hawataondoka katika barabara za jiji na kuacha kuzuia majengo ya serikali hadi pale rais atakapojiuzulu.

Marekani ambayo kupitia waziiri wa mambo ya nje John Kerry imetangaza wazi kuwa inawaongoza mkono wapinzani na atakutana na viongozi wa upinzani mjini Berlin nchini Ujerumani mwishoni mwa juma hili.

Waandamanaji wanataka Ukraine ikisaini mkatanba wa kibishara na Umoja wa Ulaya.

Hali ya usalama inaendelea kuzorota mjini Kiev nchini Ukraine, kufuatia maandamano yaliyoitishwa na upinzani, ukimtaka rais Viktor Yanukovich, ajiuzulu.

Awali rais Yanukovych aliomba mazungumzo na upinzani, lakini mazungumzo kati ya viongozi wa upinzani na wale wa serikali yaligonga mwamba huku kila upande ukiendelea kusisitiza kutotekeleza matakwa ya upande mwingine.

Kabla ya kujiuzulu, waziri mkuu wa Ukraine alitahadharisha kuhusu nchi hiyo kuwa uwanja wa vita baina ya Umoja wa Ulaya na Urusi, wakati huu ambapo maandamano yanaendelea kuhusu kukwama kwa kutiliana saini mkataba wa kibiashara baina ya Ukraine na Umoja wa Ulaya.

Nchi za Ulaya zimekua zikilani nguvu zinazotumiwa na polisi kwa kukabiliana na waandamanaji.
Mamia ya raia wamepoteza maisha tangu maandamano hayo yalipoanza.