Syria - Mapigano

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Syria mwezi January yafikia 136,000

Mashambulizi yamekuwa yakifanywa mjini Aleppo ambapo majeshi ya serikali yamelenga maeneo yanayokaliwa na waasi
Mashambulizi yamekuwa yakifanywa mjini Aleppo ambapo majeshi ya serikali yamelenga maeneo yanayokaliwa na waasi globalpost.com

Idadi ya watu waliopoteza maisha nchini Syria jumamosi baada ya ndege za kijeshi za Syria kufanya mashambulizi katika eneo la waasi jijini Aleppo imefikia 46 kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu.

Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo Rami Abdel Rahman alithibitisha vifo hivyo kutokea huku akitaja watu 33 walikuwa ni raia wa eneo la Tareq al Bab.

Shambulizi hilo linakuja siku moja baada ya waziri wa ulinzi wa syria Generali Fahd al-Freij alipozuru baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa jimbo hilo la Aleppo ambapo majeshi ya serikali yamepalenga katika siku za hivi karibuni.

Shirika la habari la Syria liliarifu kuwa waziri huyo alizuru Alepo kutoa heshima kwa wapiganaji mashujaa wa jeshi la kiarabu.

Kwa jumla shirika hilo limebainisha takwimu za mwezi january zinazoonyesha takribani watu 136,000 wamepoteza maisha nchini syria katika ghasia zilizolenga zaidi maisha ya raia.