SYRIA-Mapigano

Mapigano yanaendelea nchini Syria baada ya mazungumzo mjini Geneva

Mshambulizi ya anga yaliyofanywa na majeshi ya serikali dhidi ya mji wa Allepo unaoshikiliwa na waasi
Mshambulizi ya anga yaliyofanywa na majeshi ya serikali dhidi ya mji wa Allepo unaoshikiliwa na waasi RFI

Majeshi ya serikali nchini Syria, yamefanya mashambulizi ya anga mwishoni mwa juma lililopita katika mji wa Allepo uliotekwa na waasi baada ya mazungumzo ya Geneva Uswisi na kusababisha mauaji ya watu 121. Shirika linalo tetea haki za binadamu nchini Syria limearifu kuwa watu 36 wamepoteza maisha jana jumapili wakiwemo watoto katika mashambulio makubwa yaliotekelezwa na majeshi ya serikali katika kitongoji kimoja cha mji wa Alepo katika kata ya Tareq al Bab.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo waasi 16 wameuawa kaskazini mwa Syria katika mashambulio mawili ya kujitowa muhanga dhidi yao yaliotekelezwa na waasi wa kundi la Jihad ambao wamekuwa wakipambana tangu kipindi kadhaa, huku zaidi ya waasi ishirini wakijeruhiwa katika shambulio hilo.

Kabla ya kugeukana na kuwa maaduwi waasi hao wa kundi la Jihad walikuwa wameungana na waasi wa jeshi huru la syria kwa ajili ya kupambana na majeshi ya serikali ya rais Assad. Watu zaidi ya elfu moja na mia nne tayari wamepoteza maisha kufuatia mashambulizi hayo.

Aidha kuhusu mashambulio ya kikosi cha serikali, shirika linalo tetea haki za binadamu limesema jumla ya watu 121 wamepoteza maisha kufuatia mashambulizi ya siku ya Jumamosi na Jumapili ambapo kwa siku ya Jumamosi watu 85 waliuawa na makombora ya ndege za serikali.

Awali mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu nchini humo Rami Abdel Rahman alithibitisha vifo hivyo kutokea huku akitaja watu 33 walikuwa ni raia wa eneo la Tareq al Bab.

Shambulizi hilo linakuja siku moja baada ya waziri wa ulinzi wa Syria Generali Fahd al-Freij alipozuru baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa jimbo hilo la Aleppo ambapo majeshi ya serikali yamepalenga katika siku za hivi karibuni.

Shirika la habari la Syria liliarifu kuwa waziri huyo alizuru Alepo kutoa heshima kwa wapiganaji mashujaa wa jeshi la kiarabu.

Kwa jumla shirika hilo limebainisha takwimu za mwezi january zinazoonyesha takribani watu 136,000 wamepoteza maisha nchini syria katika ghasia zilizolenga zaidi maisha ya raia.