UKRAINE-Maandamano

Upinzani unajiandaa kufanya maandamano makubwa licha ya kutahadarishwa na serikali

Mkusanyiko uliyoitishwa na upinzani kwenye eneo liliobatizwa Uhuru,mjini Kiev nchini Ukraine, februari 2
Mkusanyiko uliyoitishwa na upinzani kwenye eneo liliobatizwa Uhuru,mjini Kiev nchini Ukraine, februari 2 REUTERS/Vasily Fedosenko

Watu yumkini 30,000 wamekusanyika jana kwenye eneo liliobatizwa Uhuru katikati ya mji wa Kiev, wakisikiliza hotuba za viongozi wa upinzani, ambao wamefahamisha kuendelea kwa siku ya leo na maandamano. Wamewatolea wito raia wote wa Ukraine kujitokeza mabarabarani mchana wa leo wakiwa na bendera ya taifa la Ukaraine, ili kuonyesha kua raia hawapumbazwi na vitisho vinavyotolewa na viongozi wa serikali.

Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo kuna watu wanaovalia kofia za chuma wa kiwa na fimbo, ambao wamekua wakipiga doria pembezuni mwa barabara iliyobatizwa Uhuru.

Katika baadhi ya mitaa ya mjini Kiev na miji mingine ya mashariki mwa Ukraine, kuna makundi ya wanamgambo, ambao vyombo vya habari vya Ukraine vinatuhumu kwamba makundi hayo yanalipwa na utawala.

Hayo yakijiri, rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch, anarejea kazini jumatatu hii baaada ya kuwa nje ya ofisi kwa muda wa siku kadhaa kufuatia likizo fupi ya kuumwa, wakati upinzani ukiendelea kukaidi wito wa kusitisha maandamano.

Rais Viktor Ianoukovitch anarejea ofisini wakati huu moja miongoni mwa tatizo kubwa kwake limepatiwa ufumbuzi na ambalo ilikuwa ni kupelekwa nje ya nchi kwa ajili ya matibabu kwa mpinzani wake mkuu Dymtro Boulatov ambaye rais anasema alitekwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana.

Dymtro Boulatov ni miopngoni mwa viongozi wakuu wanaohamasisha vuguvugu la maandamano na ambaye aliandaa mara kadhaa mgomo mbele ya ofisi za ikulu ya rais jijini Kiev.
Kiongozi huyo alitekwa tangu Januari 22 na kufanyiwa matezo kabla na kuachwa peke yake porini kabla ya polisi kumtia nguvuni na ambapo picha za kiongozi huyo zilitanda katika mitandao mbalimbali na ambapo nchi za magharibi ambazo zinaonekana kuunga mkono waandamanaji nchini humo zimeitaka serikali kuruhusu kuelekea nje ya nchi kwa ajili ya kupata matibabu, jambo ambalo limetekelezwa.

Upinzani nchini Ukraine unaituhumu serikali kuhusika na tukio hilo.
Upinzani nchini Ukraine umetangaza kwamba nchi za Magharibi hususan Marekani na Ujerumani zimekubali kutowa msaada wa fedha kwa ajili ya kusaidia katika juhudi za majadiliano na serikali.

Ukraine ilijikuta haina msaada wowote kutoka Umoja wa ulaya baada ya rais Ianoukovitch kusitisha mkataba wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya, na badala yake kupokea msaada kutoka Urusi wa Euro bilioni 15.

Hata hivyo rais wa Urusi Vladimir Poutine amebaini wasiwasi juu ya mkataba huo iwapo upinzani utachukuwa madaraka.