JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Usalama

Vikosi vya Afrika na Ufaransa vyauweka kwenye himaya yao mji wa Sibut

Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha wanajeshi kutoka mataifa ya Afrika Misca na Ufaransa wakiwalindia usalama raia, mjini Bangui
Baadhi ya wanajeshi wa kikosi cha wanajeshi kutoka mataifa ya Afrika Misca na Ufaransa wakiwalindia usalama raia, mjini Bangui RFI

Mji wa Sibut kaskazini mwa Bangui nchini jamhuri ya Afrika ya Kati umerejea jana katika mikono ya askari wa kulinda amani wa Afrika Misca pamoja na askari wa Ufaransa wa operesheni Sangaris. Vikosi hivyo vilitumwa ncjini Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kulinda amani na kupokonya silaha makundi na raia wanozimiliki.

Matangazo ya kibiashara

Baada ya siku 15 ya uporaji uliokithiri, waasi wa zamani wa Seleka waliokuwa wanashikilia mji huo wamekimbilia kaskazini na mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, jambo ambalo limepongezwa na wakaazi wa mji huo.

Vikosi hivyo vimefanikiwa kuurejesha mikononi mwao mji Sibut huo wakati huu mpango wa kuongeza nguvu katika jeshi hilo ukifanikiwa kukusanya dola za Marekani milioni 132 kutoka mataifa ya Afrika.

Kamanda wa jeshi la Umoja wa Afrika Tumenta Chomud aliimbia radio ya taifa hilo kuwa jeshi lake limedhibiti mji uliokuwa chini ya wapiganaji waasi wa kiislamu seleka waliopindua serikali mnamo mwezi machi 2013 na kulitumbukiza taifa hilo katika mzozo.

Hayo yanajiri wakati juzi jumamosi viongozi wa bara la Afrika na wanadiplomasia wa kimataifa wamefanikisha zoezi la kuchangia pesa jeshi la umoja wa Afrika chini ya operesheni yake MISCA ambayo inatarajiwa kuongeza wanajeshi takribani elfu sita kufikia mwezi machi mwaka huu.

Aidha Viongozi wa nchi za Afrika walikubaliana kuendelea kuchukua hatua zaidi kudhibiti machafuko yanayozikumba nchi wanachama sambamba na kuunda kikosi cha dharura kitakachoshughulikia migogoro inayolikumba bara hilo, azimio hilo limefikiwa jana katika siku ya mwisho ya mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Viongozi walioshiriki mkutano huo wa siku mbili wametaka kuchukuliwa kwa hatua za haraka ili kuikoa nchi ya Sudani Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo zinakumbwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti mpya wa AU ambaye ni Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz amesema nchi wanachama zitatoa wanajeshi watakaounda kikosi hicho

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa hii ni hatuwa kubwa muhimu katika kurejesha amani kwenye eneo hilo

Wakati hayo yakijiri, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji IOM limetangaza kuwasili mjini Ndjamena kwa mamia ya wakimbizi wenye asili ya Chad waliokuwa wanaishi nchini jamhuri ya Afrika ya kati na kujikuta katika hali ya ngumu kijamii kwa vile wengi bado hawajawaona ndugu zao.

Aliou KA, afisa uhamiaji wa Shirika la IOM nchini Chad, amesema wakimbizi hao wao katika hali ngumu.

“Wengi wao hawana tena ndugu hapa nchini Chad, wengi hawajui wende wapi hadi sasa, labda baadaye wataamua, hatujajua lini lakini ni maamuzi yatakayowachukuwa muda ila lazima yakafanyike, kwa sababu sijaona hata mmoja ambaye ana nia ya kurejelea hali ilivyo nchini jamhuri ya Afrika ya kati”, amesema Aliou.

Machafuko yaliyotokea nchini Jamhuri Afrika ya kasti umesababisha mamia ya watu kupoteza maisha na maia kwa maelfu kuyahama makaazi yao