JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-CHAD

Vikosi vya Chad vyatuhumiwa kuwasaidia wapiganaji wa zamani wa Seleka

RFI

Shirika la kimataifa linalo tetea haki za binadamu la Human Right Watch limetowa ripoti yake ambamo limevituhumu vikosi vya Tchad vilivyomo katika majeshi ya kulinda amani vya Umoja wa Afrika Misca kwa kuwasaidia waasi wa kundi la Seleka hasa katika kuwasaidia viongozi wa kundi hilo kutoroka.

Matangazo ya kibiashara

Human Right Watch imeomba vikosi hivyo vya Tchad kuondolewa katika majeshi ya Misca na uchunguzi uanzishwe.

Hayo yanajiri wakati juzi na jana jumatano vikosi vya Tchad vikiendesha vitisho katika mji wa Boali baada ya kwenda kuwaokowa waislam waliokuwa wamekimbilia kanisani tangu siku 15 zilizopita na kujikuta wakirusha risase dhidi ya raia wa kikristo, hali ambayo iliyozua mtafaruku katika mji huo.

Katika hatuwa nyingine wapiganaji wa kundi la Seleka wanaokadiriwa kufikia 250 wamepokelewa na jeshi la Tchad katika mpaka wa jamhuri ya Afrika ya kati na Tchad wakikimbia vita na kudai kuwa hawataki tena vita na wamepelekwa kwenye umbali wa kilometa mia sita na mpaka huo.