SYRIA

Raia wa Syria waanza kuondoka katika mji wa Homs

Moja ya familia ya raia wa Syria katika mji wa Homs, januari 30 mwaka 2014.
Moja ya familia ya raia wa Syria katika mji wa Homs, januari 30 mwaka 2014. REUTERS/Thaer Al Khalidiya

Kundi la kwanza la raia wa Syria limeondolewa likiwa ndani ya basi katika mji wa Homs, baada ya kuzuiliwa kutoondoka katika mji huo kwa kipindi cha siku 600. Raia hao wameondoka katika mji wa Homs, baada ya jeshi na waasi kuheshimisha mkataba wa usitishwaji mapigano ili kuruhu raia waishio katika maeneo mbalimbali ya mji wa Homs unaoshikiliwa na waasi na kuzingirwa na jeshi kuondoka.

Matangazo ya kibiashara

Utawala wa Bachar al-Assad umethibitisha kwamba utashiriki katika awamu ya pili ya mazungumzo na upinzani, yanayotazamiwa kufanyika februari 10 mjini Geneva, ambayo yanalenga kutafutia suluhu la kisiasa kwa mapigano yanayoendelea kuathiri taifa la Syria karibu miaka mitatu.

Mashahidi wanasema wamewaona watu 11wakipandishwa ndani ya basi. Shirika la habari la serikali Sana limetoa idadi inayofanana na hii kwamba mtoto wa kike, mwenye umri wa miaka 10 na watu wazima 10 wamepandishwa ndani ya basi na kuondoka katika mji wa Homs.

Televisheni za Syria zimeonyesha idadi kubwa ya wanajeshi karibu ya basi la kwanza, huku baadhi ya wanajeshi wakikataza wanahabari kusogelea basi hilo.
Mkuu wa mji wa Homs, Talal Barazi, amebaini kwamba zoezi hilo la kuwaondoa raia katika mji wa huo, litaendelea katika siku zijazo.

Mabasi mengi yakisindikizwa na magari yakusafirisha wagonjwa ya shirikisho la msalaba mwekundu yameingia mapema leo asubuhi katika mji mkongwe wa Homs.
“Kulingana na taarifa tuliyopewa na Umoja wa Mataifa, idadi ya watakao ondolewa leo katika mji wa Homs ni watu 200”, amesema mkuu wa mji wa Homs. Watoto wenye umri uliyochini ya miaka 15, watu wazima waliyo na zaidi ya umri wa maika 55 na wanawake wameruhusiwa kuondoka katika mji wa Homs, ameendelea kusema Talal Barazi.

Kwa mujibu wa wafuasi wa upinzani, mkataba wa usitishwaji mapigano kwa muda wa siku nne umewekwa katika vitendo ili kuruhusu zowezi hilo.

Upinzani umefahamisha kwamba utashirika mazungumzo yajayo. Hayo yanajiri wakti machafuko bado yanaendelea katika maeneo mengine.

Kwa mujibu wa shirika linalotetea haki za binadamu nchini Syria waasi walishambulia jana jela kuu linalopatikana katika mji wa Allepo (kaskazini), na kudhibiti baadhi ya majengo ya jela hilo, kabla ya jeshi kuanzisha operesheni zake na kuwatimua mapema leo asubuhi.