UFARANSA-DIPLOMASIA

Rais wa Ufaransa Francois Hollande kuanza ziara ya siku tatu nchini Marekani kuimarisha uhusiano wa kibiashara

Rais wa Ufaransa François Hollande,
Rais wa Ufaransa François Hollande, REUTERS/Benoit Tessier

Rais wa Ufaransa Francois Hollande kesho Jumatatu anaanza ziara ya siku tatu nchini Marekani, akitarajiwa kuacha kando masuala ya kshfa, wakati huu akitafuta kuinua juu mahusiano ya kibiashara na kufufua uchumi wa Ufaransa uliokwama.

Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo rais Hollande atakaribishwa kwa chakula cha jioni kwenye ikulu ya White House na kuzungumza na rais Barrack Obama kabla ya kuelekea California kukutana na viongozi wa teknolojia.

Vyanzo kutoka Ikulu ya rais jijini Paris vimeeleza kuwa ziara hiyo itaangazia zaidi uhusiano mzuri wa kikazi baina ya Ufaransa na Marekani , lakini rais Hollande pia atagusia kidogo kuhusu suala la uchunguzi wa Marekani katika mataifa ya bara Ulaya.

Aidha viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili suala la vita nchini Syria,mango wa nyuklia wa Irani, mgogoro wa kisiasa wa Ukraine na suala la uslama barani Afrika.