SUDANI KUSINI-Mazungumzo

Marekani yazinyooshea kidole cha lawama pande zinazogomba nchini Sudan Kusini

Wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini, mjini Juba, januari 7 mwaka.
Wakimbizi wa ndani nchini Sudan Kusini, mjini Juba, januari 7 mwaka. REUTERS/James Akena

Marekani imeonya na kutahadharisha juu ya mustakabali wa SUDAN Kusini na kusema kuwa serikali na upande wa waasi wanaendelea kuiweka nchi hiyo katika hali migogoro na vita kutokana na kuvunja makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yamesababisha mauaji ya watu wengi.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo ya Marekani inakuja wakati waanglizi wa hatua ya kusitishwa kwa mapigano kutoka jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika Mashariki, IGAD wakiwa nchini humo kutathimini utekelezwaji wa makubaliano hayo yaliyofikiwa mwezi uliopita kati ya wasi na serikali.

Marekani imesema kuwa inaguswa na hali ya machafuko nchini Sudan Kusini na kuzishushia lawama pande hizo mbili kutokana na kukiuka makubaliano ya Addis Ababa.

Hayo yakijiri, serikali ya Sudan Kusini imesema kuwa iko tayari kwa mazungumzo ambayo yanatarajiwa kuanza huko Addis-Ababa Ethopia na kundi la waasi kwenye juhudi za kusaka suluhu la amani ya kudumu nchini humo pia imesema kuwa kwa sasa inadhibiti majombo yote, baada ya kuyaweka kwenye himaya yake majimbo yaliyokuwa chini ya udhibiti wa waasi wanaomuunda mkono aliyekua makamo wa rais wa taifa hilo changa Riek Machar.

Lakini madai hayo yamekanushwa na upande wa waasi.