SYRIA-Mazungumzo

Mazungumzo kuhusu Syria yanaanza kwa mara nyingine tena mjini Geneva

REUTERS/Jamal Saidi

Wajumbe wa baraza la upinzani nchini Syria pamoja na wajumbe wa serikali, wanakutana tena leo katika awamu ya pili ya mazungumzo ya mjini Geneva Uswisi pamoja na mpatanishi wa Umoja wa Mataifa Lakhtar Brahimi baada ya wiki moja ya mapumziko.

Matangazo ya kibiashara

Mwezi uliyopita, kikao kiliyowakutanisha wajumbe wa serikali na upinzani kilimalizika bila hata hivo pande hizo mbili kuafikiana katika masuala ya siasa, ikiwa sasa ni miaka miatu toka nchi hio iingiye katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Mada tatu muhimu ambazo zitazungumziwa leo zitakua zilezile ziyozungumziwa katika kikao cha mwezi uliyopita : serikali ya mpito, usitishwali mapigano na hali ya kibinadamu.

Wajumbe kutoka pande mbili watakutana bila hata hivo kuzungumza moja kwa moja kama walivyofanya mwezi uliyopita, kaxzi kubwa itakua kwa msuluhishi maalumu wa Umoja wa MataifaLakhdar Brahimi.

Lakhtar Brahimi anakutana kwanza na kila upande kabla ya kukutanisha pande zote mbili kwa pamoja hapo kesho.

Katika swala kuhusu hali ya binadamu, kutazungumziwa hatua iliyo chukuliwa na serikali pamoja na waasi ya kusitisha mapigano ili kuruhusu raia waondoke katika mji wa Homs, ambao wamekua wakiziwiliwa mjini humo katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili na nusu.

Aidha kuhusu swala la usitishwaji mapigano, kutazungumziwa hali inayojiri katika jimbo la Allepo kaskazini mwa Syria, ambako jeshi la serikali limekua likishambulia kila siku kwa mabomu, na kusababisha maafa.

Lakini swala muhimu ni lile lihusulo suluhu la kisiasa. Upinzani na mataifa ya magharibi yanasisitiza iundwe serikali ya mpito ambayo itakua na madaraka thabiti, jambo ambalo litnatupiliwa mbali na serikali ya Damas.

Katika hatuwa nyingine Umoja wa mataifa UN kupitia Mkuu wa shirika la misaada ya kibinadamu la Umoja huo Valerie Amos amesisitiza kuwa mashirika ya misaada ya Umoja wa Mataifa hayatazuiliwa na mashambulizi dhidi ya msafara uliokuwa ukipeleka vifaa katika mji wa Homs nchini Syria hapo jana.

Wachambuzi wa siasa wanaona kuwa pande hizo mbili zinatakiwa kuongeza juhudi katika mazungumzo hayo ili kufikia muafaka.