BURUNDI-Mafuriko

Watu zaidi ya 50 wafariki mjini Bujumbura nchini Burundi kutokana na mafuriko

Moja ya tarafa ya mji wa Bujumbura iliyoathiriwa na mvua, februari 10 mwaka 2010.
Moja ya tarafa ya mji wa Bujumbura iliyoathiriwa na mvua, februari 10 mwaka 2010. AFP PHOTO/ESDRAS NDIKUMANA

Watu zaidi ya 51wamefariki katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, kutokana na mvua ilizonyesha usiku wa jana jumapili kuamkia leo jumamatatu, idadi ambayo haijawahi kushuhudiwa katika katika mji mkuu huo.“Mvua iliyonyesha usiku wa jana katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura, umesababisha hasara kubwa”, amesema waziri wa usalama wa raia, jenerali Gabriel Nizigama, katika mkutano na waandishi wa habari, akibaini kwamba wameshapata miili 51 ya watu waliyouawa kwa kuangukiwa na kuta za nyumba, na wengine wamkufa maji kutokana na mafuriko.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wanahofu kwamba huenda idadi hio ikaongezeka, baada ya hali hii kuyakumba maeneo mengine ya mji wa Bujumbura, lakini polisi inafahamisha kwamba mji wa Bujumbura haujawahi kushuhudiwa maafa kama hayo ambayo kutokana na mvua.

Mabarabara yanayotoka katika mji wa Bujumbura na kuelekea mikoani hayapitiki, takriban yote yameharibika kutokana na mvua hio, polisi imefahamisha kwamba watu zaidi ya mia moja wamejeruhiwa, na mamia ya nyumba zimeteketea kutokana na mafuriko.

Baadhi ya maeneo mengine ya nchi yamekumbwa na mkasa huo. Wakati huu Burundi imo katika msimu mdogo wa masika. Hata kama hakujapatikana taarifa zozote kuhusu hali inayojiri katika maeneo mengine ya nchi, mji wa Bujumbura na vitongoji vyake vimeathirika zaidi.

“ Ni kwa mara ya kwanza mji wa Bujumbura unakumbwa na hali hii”, amethibitisha meya wa manispa ya jiji la Bujumbura Saidi Juma, huku akiwatolea wito raia wa mji huo kua na mshikamano katika kipindi hiki kigumu, akiomba Jumuiya ya Kimataifa kushirikiana na viongozi wa nchi kwa kuakabiliana na majanga kama hayo.

Kwa mujibu wa waziri wa usalama, miili ya watu waliyofariki itapaswa kuzikwa mchana wa leo kutokana na kukosekana kwa sehemu ya kuhifadhi maiti katika hospitali mbalimbali za mji wa Bujumbura.

Maeneo yaliyoathirika zaidi na mvua hio ni wilaya ya Kamenge ambapo zaidi ya maiti 30 zimeokotwa, wilaya ya Buterere, eneo la Carama katika wilaya ya Kinama,eneo la Gatunguru-Gasenyi.

Kuna taarifa ambazo zinasema kwamba hata wilaya ya Isale katika mkoa wa Bujumbura (vijijini) watu 17 huenda wamefariki kutokana na mvua hio.

Asilimia 65 ya nyumba katika maeneo yaliyokumbwa na mvua hio, zimejengwa kwa tofari za udongo.

Shirika linalotetea haki za binadamu cnihi Burundi League Iteka, limefahamisha kwamba huenda idadi hio ikaongezeka kwani kuna watu, ambao wamefunikwa na vifusi.

Kiongozi wa shirika hilo Joseph Ndayizeye ameomba serikali kuchukua hatua inayopiga marufuku ujenzi wa nyumba pembezuni mwa mito au mifereji inayosafirisha maji taka