Burundi-mafuriko

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko nchini Burundi huenda ikaongezeka ambapo kwa sasa imefikia watu 60

Mafuriko nchini Burundi
Mafuriko nchini Burundi RFI/BILALI

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika mafuriko yaliotokea nchini Burundi huenda ikaongezeka kufuatia baadhi ya watu hadi sasa hawajulikani walipo.

Matangazo ya kibiashara

Duru za serikali zimearifu kwamba watu zaidi ya 50 wamepoteza maisha kufuatia mafuriko hayo yaliosababishwa na mvua kubwa zilizo nyesha katika usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu.

Hapo jana waziri wa Usalama wa raia Jenerali Gabriel Nizigama alitaja idadi ya watu 51 ndio walipoteza maisha baada ya kuangukiwa na kuta za nyumba zao na wengine kupelekwa na maji, eneo lililoa athirika zaidi ni kaskazini mwa jiji la Bujumbura.

Msemaji wa shirika la msalaba mwekundu nchini Burundi Alexis Manirakiza amesema wamehesabu miili ya watu 60 waliopoteza maisha wengi wakiwa ni watoto bila hata hivyo kutaja idadi ya watoto hao.

Polisi nchini Burundi imesema hii ni mara ya kwanza kutokea kwa maafa ya aina hii kutokana na mafuriko na hofu imetanda huenda idadi ya watu waliopoteza maisha ikaongezeka, kutokana na taarifa za mafuriko katika Miko mingine ya taifa hilo. Burundi wakati huu ipo katika msimu wake wa mvua.