SUDANI KUSINI-Mazungumzo

Waasi wa Sudan Kusini watishia kujiondoa kwenye mazungumzo iwapo Uganda haitowandoa wanajeshi wake nchini Sudan Kusini

Wajumbe wa waasi wa Sudan Kusini katika mazungumzo ya kusaka amani, januari 13 mwaka 2014 mjini Addis-Ababa
Wajumbe wa waasi wa Sudan Kusini katika mazungumzo ya kusaka amani, januari 13 mwaka 2014 mjini Addis-Ababa AFP/ Carl de Souza

Serikali ya Ethiopia ambayo inasimamia mazungumzo ya waasi wa Sudani Kusini na serikali ya rais Salva kiir imetowa wito wa kuondolewa kwa majeshi ya Kigeni nchini Sudani Kusini hususan majeshi ya Uganda kwa hofu ya kuufanya mzozo huo kuwa wa kikanda.

Matangazo ya kibiashara

Waasi wa Sudani Kusini wametishia kujiondowa kwenye mazungumzo hayo iwapo wanajeshi wa Uganda wataendelea kutekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vyao.

Majeshi ya Uganda yaliingia nchini Sudani Kusini kufuatia ombi la rais Salva Kiir kukabiliana na waasi.

Taban Deng mjumbe wa waasi kwenye mazungumzo hayo amesema katika taarifa iliotolewa jana kwamba watajiondowa kwenye mazungumzo hayo iwapo majeshi ya Uganda yatasalia nchini Sudani Kusini huku akitowa wito wa kuachiwa huru wafungwa wanne ambao bado wanazuiliwa katika jela moja jijini Juba.

Taifa changa la Sudan Kusini limekua katika mapigano kati ya jeshi la serikali na waasi wanaomuunga mkono aliekua makamu wa rais Salva Kiir, Riek Machar, tangu desemba 15 mwaka jana.

Mapigano hayo yalisababisha mamia ya raia kupoteza maisha na mamia kwa maelfu wamelazimika kuyahama makaazi yao.

Mazungumzo yanayoendelea mjini Addis-Ababa, nchini Kenya yameanzishwa kwa jitihada za Jumuiya ya Kikanda ya maendeleo ya Afrika ya Mashariki IGAD.

Awali serikali ya Uganda ilikataa katu katu kwamba haikuwatuma wanajeshi wake nchini Sudan Kusini, lakini siku chache baadae, serikali hio ilikiri kuwatuma wanajeshi wake kwenye aridhi ya Sudan Kusini ili kusidia jeshi la seikali linalomuunga mkono rais Salva Kiir.