SYRIA-Mapigano

Jeshi la Syria laendesha mashambulizi katika mji muhimu wa Yabroud

Moja ya vijiji viliyochambuliwa na jeshi la anga la Syria
Moja ya vijiji viliyochambuliwa na jeshi la anga la Syria RFI

Jeshi la anga la Syria, kwa mara ya kwanza limeendesha mashambulizi zaidi ya kumi mapema leo katika mji wa Yabroud, karibu na mji mkuu wa Syria, katika jimbo muhimu la Qalamoun, wakaazi wa mji huo wamethibitisha. “ kumetokea mashambulizi 13 ya anga katika mji wa Yabroud na vitongoji vyake” limesema shirika linalotetea haki za binadamu la Syria (OSDH), bila hata hivo kutoa taarifa zaidi.

Matangazo ya kibiashara

Mashahidi waliyoongea na shirika la habari la AFP, wamefahamisha kwamba jeshi la Syria limeanzisha mashambulizi ili kuuweka katika himaya yake mji wa Yabroud.

“Mashambulizi ya anga yanakakwenda sambamba na mashambulizi ya aridhini”, wameendelea kusema mashahidi.

Duru za kiusalama nchini Syria zimelielezea shirika la habari la AFP kwamba mashambulizi hayo “ni katika operesheni kabambe ya kuyasaka makundi ya kigaidi yenye silaha”.

Neno “gaidi” linamanisha katika kauli za viongozi wa Syria, wapinzani pamoja na waasi wa Syria.

Duru kutoka jeshi la Syria, ziliyotolewa na shirika la habari la serikali Sana, zinafahamisha kwamba jeshi “limekithibiti kijiji cha Jarajir na maeneo mengine jirani”, karibu na kijiji cha Aarsal kinachopatikana nchini Libanon, na kuwaua magaidi magaidi waliyokua waksalia katika maeneo hayo.

Yabroud ni mji muhimu unaopatikana katika jimbo la milima la Qalamoun karibu na mpaka na Libanon, na unapatikana kwenye barabara muhimu inayounganisha miji ya Damas na Homs. Yabroud umekua chini ya uthibiti wa waasi, na ni moja ya miji mitatu iliyoathiriwa na vita nchini Syria.

Les violences ont contraint des familles de Yabroud, Flita, et Jreijer à fuir vers le village libanais d'Aarsal, a indiqué Dana Sleiman, du Haut-Commissariat des réfugiés (HCR), via Twitter.

“Mapigano hayo mapya yamesababisha mamia kwa maelfu ya ya wakaazi wa Yabroud, Flita naJreijer kukimbilia katika kijiji cha Aarsal nchini Libanon, amesema kupitia mtandao wa kijamii wa Twiter”, Dana Sleiman, afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (HCR).