Syria - Mapigano

Mpango wa kuwaondoa raia wa Syria waliyokwama katika mji wa Homs unaendelea

Raia wakiondolewa katika mji wa Homs chini ya ulinzi mkali wa Umoja wa Mataifa
Raia wakiondolewa katika mji wa Homs chini ya ulinzi mkali wa Umoja wa Mataifa AFP

Juhudi za kuwaokoa raia wa Syria waliokwama kwenye mji unaodhibitiwa na waasi wa Homs zilirejelewa tena siku ya jumatano, Jumla ya watu 217 waliokwama kwa zaidi ya miezi 18 waliondoka jana baada ya zoezi la kuwaokoa kwenye mji huo kuahirishwa siku iliyopita. Idadi ya raia walioondolewa kihalali kwenye mji mpaka sasa imefikia zaidi ya 1400.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amesema misaada ya kibinadamu imeendelea kufikishwa kwenye mji huo ili kuwasaidia waathirika wa mapigano.

Wakati huo huo mazungumzo ya amani kuhusu Syria yameendelea mjini Geneva Uswisi, huku wapinzani wakiendelea kushinikiza uundwaji wa serikali ya mpito. Lakini serikali ya Damascus ikisisitiza ni lazima majadiliano hayo yafuate utaratibu kulingana na ajenda zilizopangwa.

Wachambuzi wa maswala ya siasa wanaona kuwa wasuluhishi wa mgogoro huo wanapaswa kuipa nafasi serikali ya Syria kueleza namna wanavyotaka suluhu ya mgogoro huo ipatikane.

Msuluhishi wa kimataifa katika mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi anakutana leo na wawakilishi wa Marekani na Urusi katika mji wa Uswisi, na hakutakueko na mazungumzo kati ya utawala wa Syria na upinzani, kwa mujibu wa taarifa ziliyotolewa na wajumbe kutoka pande mbili katika mzozo wa Syria.

Hayo yakijiri mapigano yanaendelea kushuhudiwa tangu yaanzishwe nazungumzo januari 22 mwaka huu.

Jeshi la Syria limeanzisha mashambulizi karibu na mji wa Damas, likijaribu kuuweka katika himaya yake eneo la Yabroud linalopatikana katika mji muhimu wa Qalamoun unaoshikiliwa na waasi.