MISRI-URUSI-Diplomasia

Rais wa Urusi aunga mkono kugombea kwa kiongozi wa majeshi wa Misri kwenye kiti cha urais

Picha ya zamani ya kiongozi wa majeshi nchini Misri, Abdel Fattah al-Sisi (kulia) akimpokelewa waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu (kushoto), mbele ya jengo la wizara ya ulinzi nchini Misri  Reuters
Picha ya zamani ya kiongozi wa majeshi nchini Misri, Abdel Fattah al-Sisi (kulia) akimpokelewa waziri wa ulinzi wa Urusi, Sergei Shoigu (kushoto), mbele ya jengo la wizara ya ulinzi nchini Misri Reuters Reuters

Rais wa Urusi Vladimir Poutine, ameunga mkono leo kugombea kwa kigogo wa Misri, kiongozi wa majeshi ya Misri Abdel Fattah al-Sissi, ambaye yuko ziarani mjini Moscow, wakati ushirikiano kati ya Misri na Marekani unaonekena kutoshamiri. “Najua kwamba ulichukua msimamo hivi karibuni wa kugombea kwenye kiti cha urais katika uchaguzi ujao”, Poutine amemueleza Sissi.

Matangazo ya kibiashara

“Ni uamzi thabiti wa mtu kama kiongozi wa kusimamia majukumu kwa niaba ya raia wa Misri. Je vous souhaite, nikianzia kwa jina langu na raia wa Urusi, tunakutakia ushindi katika uchaguzi huo”, ameongeza rais Poutine.

“Hali ya utulivu na usalama katika mashariki ya kati inatokana kwa sehemu kubwa na hali ya utulivu ya nchi ya Misri. Nina matumaini kulingana na ujasiri na uzowefu ambao unao, utawaweka wafuasi wako sawa wakupigiye upato ili ushinde, na uwe na uhusiano mzuri na raia wengine wa Misri”, ameendelea kusema rais wa Urusi.

Waziri huyo wa ulinzi wa Misri ana wafuasi wengi, hata kama hajatangaza rasmi kwamba atagombea, lakini amekua akikaririwa kwamba atagombea kwenye kiti cha urais tangu alipompindua rais Mohamed Morsi julai 3 mwaka 2014.

Abdel Fattah al-Sissi aliwasili nchini Urusi jana jumatatu akishirikiana katika ziara hio na waziri wa mambo ya nje wa Misri Nabil Fahmi.

Viongozi hao wa Misri, walipokelewa na wenyeji wao wa Urusi Sergueï Choïgou na Sergueï Lavrov katika hali ya kudumisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili mkiwemo kijeshi.