UGANDA-MAREKANI-Diplomasia

Barack Obama amtaka Museveni Kufutilia mbali mswaada unapinga mapenzi ya jinsia moja.

Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani, Barack Obama RFI

Rais wa Marekani Barrack Obama amemuonya rais wa Uganda Yoweri Museveni kuwa ikwa atasaini mswada wa sheria mpya unaopiga marufuku ndoa ya jinsia moja nchini humo, uhusiano kati ya mataifa hayo mawili utaharibika. 

Matangazo ya kibiashara

Mswada huo uliopitishwa na bunge mwishoni mwa mwaka uliopita unasema kuwa yeyeote atayebainika kuhusika na vitendo vya ndoa ya jinsia moja atafungwa maisha jela.

Sheria hii pia inasema kuwa yeyote ambaye hatatoa ripoti kuhusu watu waliyojihusisha na ndoa hii watachukuliwa hatua.

Rais Obama anasema kuwa kutia saini kwa mwada huo ni ukiukwaji wa haki za Binadamu.

Chini ya sheria hiyo iliyopendekezwa, watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ushoga watakabiliwa na hukumu kali, ikiwemo kifungo cha maisha jela.

Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani, Susan Rice, amesema kwenye mtandao wa Twitter kwamba amefanya mazungumzo ya kina na rais Museveni jumamosi usiku kumtaka asitie saini mswada huo.

Hata hivo rais Obama amekemea vikali visa vya mashambulizi na kuteswa kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, ambavyo vimeenea katika mataifa kadhaa kutoka bara la Asia hadi hadi Afrika.