NIGERIA-BOKO HARAM-Usalama

Kundi la Boko haram latekeleza mauaji ya watu zaidi ya tisini nchini Nigeria

Wanagambo wa Kiislamu wa Boko Haram nchini Nigeria wamevamia kijiji kimoja Kaskazini mwa nchi hiyo mwishoni mwa juma lililopita na kutetekeleza mauji ya zaidi ya watu 90. Walioshuhudia mauji hayo wanasema wanagambo hao walikuwa wamejihami kwa silaha hatari na walimpiga risaisi kila waliyekutana naye katika kijiji cha Izghe katika jimbo la Borno.

Uharibifu unaotekelezwa na kundi la Boko haram nchini Nigeria
Uharibifu unaotekelezwa na kundi la Boko haram nchini Nigeria FRANCE 24
Matangazo ya kibiashara

Seneta wa jimbo la Borno, Ali Ndume amesema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha huenda ikawa juu.

Inadaiwa kuwa zaidi ya wanamagmbo 100 wa Boko Harama walitekeleza mauji hayo katika jimbo hilo ambalo limeendelea kushudia ukosefu wa usalama kwa kipindi kirefu sasa.

Wanajeshi tisa waliuliwa katika jimbo hilo juma lililopita na kujiondoa katika eneo hilo suala amabalo wachambuzi wa mswala ya usalama wanasema imechangia kwa ukosefu wa usalama.

Kundi la Boko Haram limetekeleza mauji ya maelfu ya watu Kaskazini mwa nchi hiyo tangu mwaka 2009 katika harakati zao za kutaka kujitawala Kaskaizni mwa Nigeria.