ETHIOPIA-USWISI-Usalama

Ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines imetekwa nyara

Serikali ya Ethiopia imethibitisha leo jumatatu kwamba inawasiliana na shirika la ndege la Ethiopian Airlines ili kujaribu kufahamu kilichotokea kwa rubani msaidizi hadi kumlazimisha rubani wa ndege ya shirika hilo ambayo ilikua inatokea Addis-Ababa ikielekea Roma, kutua mjini Geneva. “Nina wasiliana na mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Ethiopian Airlines ili kujua kwa kina kilichotokea kwa rubani msaidizi”, waziri wa habari, Redwan Hussein amelielezea shirika la habari la AFP.

Ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines ambayo imelazimimishwa kutua mjini Geneva (nchini Uswisi), februari 17 mwaka 2014
Ndege ya shirika la ndege la Ethiopian Airlines ambayo imelazimimishwa kutua mjini Geneva (nchini Uswisi), februari 17 mwaka 2014 DENIS BALIBOUSE / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri amethibitisha kwamba rubani huyo msaidizi ni raia wa Ethiopia, mwenye umri wa zaidi ya miaka thelathini, lakini hakutaka kutoa taarifa zaidi.

“Hakuna shambulizi lolote liliyotokea aidha vitisho dhidi ya abiria, kwani ilikua kati ya rubani na rubani msaidizi”, ameendelea kusema Redwan Hussein.

Ndani ya ndege hiyo aina ya Boeing 767, kulikuemo abiria 202, wengi wao wakiwa ni raia wa Itali, na wafanyakazi wa ndege hio, amethibitisha msemaji wa mamlaka ya uwanja wa ndege, Bernard Stämpfli.

Rubani msaidizi, mwenye umri wa miaka 31, alimfungia chooni rubani kabla ya kugeuza njia iwaliyokua wakielekea na kutua kwenye uwanja wa mjini Geneva.

Rubani huyo msaidizi hakua na silaha, lakinio amesema kwamba amekua akifanyiwa vitisho nchini mwake Ethiopia, na ameomba hifadhi kama mkimbizi wa kisiasa nchini Uswisi ,polisi nchini Uswisi imethibitisha.

Mamlaka ya uwanja wa ndege mjini Geneva imefahamisha kwamba muhusika mwenyewe ndiye aliifahamisha mamlaka hio kwamba ndege yao imetekwa nyara na mtu asiejulikana, na baadae ndege ya kijeshi ya Itali ikaifuata angani, na kulazimika kutua mjini Geneva.

Baada tu ya kutua kwenye uwanja wa mjini Geneva, mtekaji nyara alitoka ndani ya ndege akipitia dirishani kwa kutumia kamba, na kujisalimisha, imesema polisi.

Polisi na vyombo husika vinatazamiwa kumhoji mtekaji nyara huyo, lakini “kisheria kosa hilo ni utekaji nyaran na adhabu yake ni hadi miaka 20 jela”, amesema mkuu wa mashtaka wa mjini Geneva.

Ndege hio iliondika jana usiku mjini Addis-Ababa, na ingelipaswa kutua mjini Roma mapema leo.

Polisi nchini Uswisi imefahamisha kwamba imemshikilia mtekaji nyara huyo, ambaye ni rubani msaidizi.

Ethiopian Airlines imebaini kwamba abiria wote na timu nzima ya wafanyakazi katika ndege hio wawako sako salama.