UKRAINE-Maandamano

Waandamanaji nchini Ukraine waondoka kwenye ukumbi wa manispa ya jiji na majengo mengine ya serikali

Waandamanaji wakiwa mbele ya ofisi za manispa ya jiji la Kiev februari 16 mwaka 2014
Waandamanaji wakiwa mbele ya ofisi za manispa ya jiji la Kiev februari 16 mwaka 2014 AFP/Sergei Supinsky

Hatimaye Waandamanaji mjini Kiev nchini Ukraine wamekubali kuondoka kwenye ukumbi wa jiji hiyo jana Jumapili , baada ya kulidhibiti jengo hilo kwa zaidi ya miezi miwili kama sehemu ya kutamatisha machafuko yaliyolenga kupinga serikali ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jengo hilo lililopo katikati mwa mji wa Kiev, limekuwa na shughuli nyingi mchana na usiku, tangu lilipokuwa makao makuu ya mapinduzi, baada ya waandamanaji waliojaribu kumwondoa madarakani Rais Viktor Yanukovych kulishambulia kwa mawe mwezi Desemba, mwaka Jana.

Inaarifiwa kuwa hatua ya kuondoka katika jengo hilo ilitekelezwa kufuatia mamlaka nchini humo kukubali kuawachia huru baadhi ya watu wote waliokuwa wanazuiliwa kutokana na machafuko hayo.

Haya yanajiri wakati Sheria ya msamaha kwa waliotenda uhalifu na makosa mengine inaanza kutekelezwa hii leo Jumatatu nchini Ukraine.

“Sheria hio inaanza kutekelezwa leo jumatatu, na inatazamiwa kufuta kesi zote za watu waliyotenda maovut tangu mwaka jana desemba 27 hadi februari 2 mwaka huu”, imethibitisha ofisi ya mashtaka.

Hatua hii inakuja baada ya waandamanaji kuondoka kwenye ukumbi wa manispa ya jiji na majengo mengine ya serikali mikoani.

Watu takriban 700 walikua wakianadamana mchana na usiku kucha mbele ya ukumbi huo wa manispa ya jiji tangu maandamano hayo yalipoanza zaidi ya miezi miwili iliyopita.