SUDANI KUSINI-Mapigano

Mapigano yazuka nchini Sudani kusini

Wanawake wakiyakimbia mapigano katika mji wa Malakal, nchini Sudani kusini
Wanawake wakiyakimbia mapigano katika mji wa Malakal, nchini Sudani kusini RFI

Waasi wa Sudan Kusini wameanzisha mapigano ili kuudhibiti mji muhimu wa Malakal ambao uko chini ya himaya ya jeshi la serikali, na kupelekea kuvunjika kwa mkataba wa usitishwaji mapigano kati ya jeshi na waasi uliyoafikiwa mwishoni mwa mwezi wa januari.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la serikali linafahamisha kwamba lilihofia tangu jana kutokea kwa mapigano hayo, ambayo yamekuja kuvunja mkataba wa usitishwaji mapigano uliyosinia kati ya serikali ya Juba na waasi wa wanaomuunga mkono aliyekua makamu wa rais Riek Machar.

Milio ya risase imekua ikisikika mchana kutwa leo katika mji wa Malakal, na haijajulikana nani ambaye anadhibiti mji huo, ambao ni mji mkuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Nil (kaskazini mashariki ya taifa hilo changa).

“Mapigano ni makali. Kuna mapigano katika vitongoji vya mji. Ni shambulizi kubwa”, limethibitisha shirika moja la kihisani, likibaini kwamba ndege za kivita zimekua zilizunguuka eneo la mapigano.

Msemaji wa jeshi, Philip Aguer, amethibitisha shambuliyo hilo, bila hata hivo kufahamisha anaedhibiti mji wa Malakal.

“ Ni dhahiri kwamba waasi hawaheshimu mkataba wa usitishwaji mapigano, hawako tayari kusikia mchakato wa amani, wanafikiri kwamba suluhu inapatikana kwa mtutu wa bunduki”, amesema Michael Makuei, kiongozi wa ujumbe wa serikali katika mazungumzo ya kusaka amani na waasi mjini Addis-Ababa.

Msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (Minuss) amesema vituo vya Umoja wa Mataifa nchini humo, kulikokimbilia maefu ya wakimbizi wa ndani vilionekana tupu kutokana na mapigano hayo yaliyozuka mapema leo asubuhi.

“Kuna habari zinasema kwamba soko la mji wa Malakal linawaka moto, na huenda waasi wameshaingia katika mji huo”, limesema shirika lingine la kihisani.

Sudan Kusini imekumbwa na mapigano kati ya jeshi linalomuunga mkono rais Salva Kiir na waasi wanaomuunga mkono Riek Machar tangu desemba 15.

Mapigano hayo yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine karibu 900,000 kuyakimbia makaazi yao, mapigano ambayo yalianza katika mji wa Juba , na baadae kuenea nchi nzima, katika majimbo ya Nil, Jonglei (mashariki) na Unity (kaskazini).