THAILAND-Usalama

Thailand: Waandamanaji wakamatwa mjini Bangkok

Waandamanaji wakijaribu kupambana na kikosi cha kuzima fujo mjini  Bangkok, februari 17 mwaka 2014
Waandamanaji wakijaribu kupambana na kikosi cha kuzima fujo mjini Bangkok, februari 17 mwaka 2014 REUTERS/Chaiwat Subprasom

Viongozi nchini Thailand wameamuru polisi kuanzisha leo jumanne operesheni kabambe ili waweze kurejesha kwenye himaya ya serikali maeneo mengi ambayo yameshikiliwa na waandamanaji kwa miezi kadhaa sasa. Askari polisi mmoja ameuawa. Waziri mkuu Yingluck Shinawatra amezungumza kupitia televisheni msimamo wa serikali.

Matangazo ya kibiashara

Askari polisi wengi wameonekana tangu saa moja asubuhi saa za Bangkok katika baadhi ya maeneo, na tayari eneo moja kati ya maeneo yanayoshikiliwa na waasi, liliyokaribu na jengo la wizara ya nishati, limerejeshwa kwenye himaya ya serikali. Mamia ya waandamanaji wamekamatwa.

Waandamanaji katika moja ya maeneo ya kaskazini ya mji wa Bangkok wanaoongozwa na mmoja wa viongozi wa madhehebu ya kibudisti Luang Pu Buddha Issara, wamekubali, baada ya mazungumzo, kuondoka katika eneo walilokua wakishikilia tangu mwanzoni mwa mwezi wa januari.

Hali ya sintofahamu imeripotiwa mapema leo asubuhi kwenye makao makuu ya serikali katika eneo la kihistoria la Bangkok.

Asikari polisi wa kuzima fujo wamevurumisha mabomu ya kutoa machozi na kufyatua risasi za plastiki ili kujaribu kutawanya kundi moja la waandamanaji lenye msimamo mkali lilokua limeweka barabarani vizuizi vya mifuko ya mchanga na vyuma.

Baadhi ya waandamanaji wamejibu kwa kufyatua risase za moto.

Watu wengi wamejeruhiwa kutoka pande zote mbili, akiwemo askari polisi mmoja ambae alipigwa risase kichwani.

Hayo yakijiri, waziri mkuu Yingluck Shinawatra ametoa tangazo rasmi kupitia televisheni. Amewataka wakulima wa mchele, ambao wamekua wakiandamana mjini Bangkok wakidai marupurupu ya mishahara, akibaini kwamba operesheni hio haiwalengi wakulima hao