JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Usalama

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Milio ya risase yautikisa mji wa Bangui

Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) katika kata ya Boy-rabe, makao makuu ya wanamgambo wa anti-balaka, mjini Bangui, februari 19 mwaka 2014 ...
Wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) katika kata ya Boy-rabe, makao makuu ya wanamgambo wa anti-balaka, mjini Bangui, februari 19 mwaka 2014 ... FRED DUFOUR/AFP

Milio ya risase za rashasha na miripuko ra roketi na gruneti imesikika mapema leo asubuhi karibu na uwanja wa ndege wa mjini Bangui, ambako waandamanaji wameweka vizuizi dhidi ya vikosi vya kimataifa, ameshudia muandishi wa AFP.

Matangazo ya kibiashara

Risase zimerushwa hadi karibu na kambi ya wanajeshi wa Ufaransa wanaolinda eneo moja la uwanja wa ndege, na wako tayari kujibu mashambulizi yoyote dhidi yao, milio hiyo ya risase imesababisha watu kua na hofu katika maeneo jirani ya uwanja wa ndege.

Duru za kijeshi zinafahamisha kwamba milio hio inashukiwa kwamba huenda ni ufyatulianaji risae kati ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) na wanamgambo wa kundi la wa kristo la anti-balaka wanaoishi karibu na maeneo jirani na uwanja wa ndege.

Mamia ya watu wanaoishi katika kambi kubwa ya wakimbaizi wa ndani iliyo karibu na uwanja wa ndege, wamekimbilia sehemu ndege zinaegesha baada ya kutua, lakini wanajeshi wa Ufaransa wameingilia kati na kuomba watu hao kurejea kambini.

Makundi madogo madogo ya watu, ambao wamekua wakiandamana wakipinga operesheni ya wanajeshi wa Ufaransa dhidi ya wanamgambo wa kundi la ant-balaka, wameweka vizuizi kwenye barabara inayoelekea kwenye uwanja wa ndege.

Kwenye umbali wa mita zaidi ya mia moja na ua wa uwanja wa ndege, vijana kati ya 200 na 300wamekua wakipaza sauti wakilani operesheni (Sangaris) inayoendeshwa na wanajeshi wa Ufaransa na ile ya wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Misca) pamoja na siasa ya viongozi wa srikali ya mpito.

Milio ya risase imesikika pia jana usiku hadi mapema leo asubuhi katika kata ya Boy-Rabe, makao makuu ya wanamgambo wa anti-balaka, na katika eneo la kaskazini mwa mji.

Moja kati ya mpango wa rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ni kuhakikisha usalama umerejea nchini, na alahidi kuanzisha vita dhidi ya wanamgambo wa kundi la anti-balaka.

Mapigano hayo mapya yamesababisha ujumbe wa viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wanahirisha ziara ambayo wangeifanya leo jumatano katika mji wa Bossangoa ( kilomita 250 kaskazini magharibi na mji wa Bangui).