UKRAINE-Maandamano

Makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yanaendelea kushuhudiwa nchini Ukraine

Genya Savilov/AFP

Askari wa kutuliza ghasia wameanzisha mashambulizi mapya mjini Kiev dhidi ya waandamanaji, kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi. Askari polisi hao wanaotumia nguvu kuwatawanya waandamanaji sasa wamelizingira eneo maarufu la mnara wa Maidan.

Matangazo ya kibiashara

Katika mashambulizi yaliyofanyika jana, watu wasiopungua 16 wameripotiwa kuuwawa wakiwemo waandamanaji wanne wa mnara wa Maidan uliodhibitiwa na waandamanaji hao kwa takriban miezi mitatu sasa.

Aidha, katika jitihada za kufikia makubaliano kati ya wapinzani wa serikali ya rais Viktor Yanukovych na baada ya mazungumzo na wajumbe wao, “msimamo wa rais huyo haukubadilika kwa vile amesema kuwa hatozuia opersheni hiyo”, amesema mpinzani Vitali Klitschko baada ya mkutano na rais.

Upinzani nchini Ukraine unakosoa uhusiano wa serikali ya Yanukovych na nchi ya Urusi na badala yake kupendelea makubaliano yafanyike baina ya serikali hiyo na Umoja wa Ulaya.

Hivi kaibuni upinzani nchini Ukraine uliiomba serikali ya Ujerumani kuwapa msaada wa kifedha na kuiadhibu serikali ya rais Viktor Ianoukovitch , na washirika wake kwa kile wanachokisema kuwa inaendelea kukuza unyanyasaji wa kisiasa licha ya kukubali utekelezwaji wa mpango wa msamaha kama walivyoafikiana.

Katika Mazungumzo yao na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin
Upinzani huo uliitaka serikali hiyo ya ujerumani kuzingatia madai waaliyokuwa wamependekeza huku Merkel akisema kuwa itabidi Umoja wa Ulaya kukutana katika mkutano wa dharura kujadili suala zima la Ukraine, Katika Siku za hivi karibuni.

“Nina imani kwamba Umoja wa Ulaya na Ujerumani wana mpango wa kuuchukulia vikwazo utawala wa Viktor Ianoukovitch” alisema Vitali Klitschko gwiji wa zamani wa ndondi aliejinyakulia sifa nyingi nchini Ujerumani, ambae pia ni mmoja kati ya viongozi wa upinzani wa Ukraine katika kikao na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel mjini Berlin.

Vitali Klitschko na Arseni Iatseniouk, ambaye ni mshirika wa karibu wa mmoja wa wapinzani anae ziwiliwa, Ioulia Timochenko, walipokelewa juzi kwa mazungumzo na bi Merkel wakati maandamano yakiendelea kushuhudiwa nchini Ukraine, na kusababisha kuendelea kwa mzozo wa kisiasa.

“Hali inaendelea kua mbaya zaidi nchini Ukraine”, alisema bi Merkel, huku akitolea wito utawala wa Viktor Ianoukovitch kuunda serekali ya umoja na kuendelea na mchakato wa kurekebisha baadhi ya vipengele vya katiba ambavyo vinawakandamiza wapinzani.