THAILAND-Maandamano

Polisi nchini Thailand yaonywa kutotumia nguvu kwa kuzima maandamano

Kikosi cha kuzima fujo kikikabiliana na waandamanaji mjini Bangkok
Kikosi cha kuzima fujo kikikabiliana na waandamanaji mjini Bangkok AFP - Pornchai Kittiwongsakul

Majaji katika Mahakama kuu nchini Thailand imewaonya Polisi nchini humo kuwaomba kwamba wasitumie Nguvu kupita kiasi kuvunja maandamano ya amani, wakati huu waandamanaji mjini Bangkok wakisisitiza kuongeza shinikizo kumng'oa madarakani waziri mkuu Yingluck Shinawatra.

Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo la mahakama linatolewa ikiwa imepita siku mbili toka nchi hiyo ishuhudie makabiliano mabaya zaidi kati ya polisi na waandamanaji ambapo watu watano wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mpaka sasa zaidi ya watu kumi na sita wamepoteza maisha kwa pande zote mbili toka kuanza kwa maandamano hayo miezi mitatu iliyopita ambapo hivi karibuni watu wengi wamekuwa wakijeruhiwa kutokana na risasi na mabomu ambapo kila upande unamtuhumu mwenzake kutumia silaha za hatari.

Hayo ni baada ya viongozi nchini Thailand kuamuru polisi kuanzisha juzi jumanne operesheni kabambe ili waweze kurejesha kwenye himaya ya serikali maeneo mengi ambayo yameshikiliwa na waandamanaji kwa miezi kadhaa sasa.