Ukraine

Utawala wa Viktor Ianukovich unaendelea kuonywa kwa kuendelea na makabiliano dhidi ya waandamanaji

Genya Savilov / AFP

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Ujerumani na Poland wamekua wanatarajiwa leo asubuhi katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev, kabla ya mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels, huko rais wa Ukraine Ianukovich akitangaza kusitishwa kwa makabiliano kati ya kikosi cha kuzima fujo na waandamanaji, baada ya mchafuko yaliyosababish watu 26 kupoteza maisha mjini Kiev.

Matangazo ya kibiashara

 

Utawala wa Ukraine ulitangaza jana kuwachukulia waandamanaji wenye msimamo mkali hatua dhidi ya magaidi, wakati Ufaransa na Ujerumani wakiahidi kuchukulia vikwazo wahusika wote katika machafuko hayo yanayoendelea.

Rais wa Ukraine Viktor Ianukovich ametangaza kusitishwa kwa makabiliano kati ya polisi na upinzani kabla ya mawaziri hao wa Ulaya na kiongozi wa ngazi ya juu wa Urusi kuwasili mjini Kiev.

Katika hotuba yake usiku wa jumanne kuamkia jana jumatano, wakti polisi walikua tayari kuanzisha operesheni ya kuvunja maandamano katikati ya mji wa Kiev, rais wa Ukraine, alitoa msimamo wake dhidi ya upinzani na kuutuhumu kwamba wanapanga njama za kukuabiliana dhidi ya jeshi na kuipindua serikali na kuwatahadhari kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Urusi imelani maandamano yanayoendelea nchini Ukraine na kubaini kwamba ni “njama za kutaka kuipindua serikali”.

Rais Barack Obama ameounya utawala wa Ianukovich kuendelea kuvunja haki ya raia kuandamana, akibaini kwamba raia wana haki ya kuandamana, ni kwa serikali kuwalindia usalama, kuliko kuwahatarishia usalama.

Marekani imewawekea vikwazo vya kuwanyima viza viongozi 20 wa ngazi za juu wa Ukraine, ambao inawatuhumu kwamba wanahusika katika machafuko yanayoendelea mjini Kiiev, amesema mwanadiplomasia mmoja wa Marekani.

Jumuiya ya mataifa ya kujihami ya NATO, imeonya utawala wa Ukraine kuvunjika kwa uhusiano wa kidiplomasia iwapo jeshi litaingilia kati kwa kukabiliana na waandamanaji wa upinzani.