SUDAN KUSINI-Mapigano

Waasi wa Sudan Kusini wadai kuuteka mji wenye utajiri wa mafuta wa Malakal

afp.com - Carl de Souza

Waasi wanaongozwa na aliyekuwa makamu wa rais wa Sudan Kusini Riek Machar wanasema wameuteka mji wa Malakal katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile baada ya mapigano ya siku mbili na wanajeshi wa serikali. Lakini taarifa hii bado haijathibitishwa na serikali.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa kweli mji huu wenye utajiri utakua umetekwa na waasi, itakua mara ya kwa waasi hao kuuteka mji huu muhimu kwa uchumi wa Sudan Kusini baada ya makabiliano kati yao na serikali ya Juba kuanza miezi miwili iliyopita na jana jeshi la serikali lilisema lilipoteza mawasiliano na wanajeshi wake katika mji huo.

“Sina mawasiliano na uongozi wa jeshi katika mji wa Malakal”, msemaji wa jeshi Philip Aguer ameimbia AFP, akibaini kwamba waasi bado wanadhibti eneo ndogo la kusini mwa mji, “lakini eneo la mafuta bado linashikiliwa na jeshi”, amesema aguer.

Marekani, ambae ndie msimamizi wa uhuru wa Sudan Kusini katika mwaka 2011, imefahamisha jana jioni kwamba kumekua na ukiukwaji “mkubwa” wa mkataba wa usishwaji vita.

“Tunalani uvunjwaji mkubwa wa mkataba wa usitishwaji mapigano uliyo afikiwa na pande mbili husika, na pande zote hizo zimehusika katika uvunjwaji huo wa mkataba, kawa hio tunaomba mapigano hayo yakomeshwe mara moja”.

Amesema naibu msemaji wa serikali ya Marekani, Marie Harf.

Umoja wa Mataifa umefahamisha kwamba watu kumi, ikwa ni wakimbizi wa ndani, wameuawa katika mji wa Malakal, kufuatia mapigano ya “kikabila”.

Kwa mujibu wa mashirika ya kihisani, uwanja wa ndege wa Malakal ulifungwa jana jioni. Waasi wamekua wakionekana jana jioni katika mji huo, ambao ni mji mkuu wa jimbo la Jonglei, lakini haijafahamika kwamba wao ndio wana udhibiti.

Msemaji wa waasi, Lul Ruai Koang, amefahamisha kwamba wamewatimua hadi msituni wanajeshi watiifu kwa serikali ya Juba.

Amenyooshea kidole cha lawama jeshi la serikali kwamba ndio walianza kuvunja mkataba wa usitishwaji mapigano, baada ya jeshi kushambulia ngome zao, wao walichokifanya ilikua kujihami, amesema Ruai Koang.

Waasi na serikali ya Juba wamekua wakishtumiana kila upande kwamba unakiuka mkataba wa usitishwaji mapigano.

Hayo yakijiri majeshi ya Uganda ambayo yamekuwa nchini humo kusaidiana na wanajeshi wa Juba wanatarajiwa kuondoka nchini humo ndani ya miezi miwili ijayo kutokana na shinikizo kutoka kwa Marekani kuondoka nchini humo.