UKRAINE-UMOJA WA ULAYA- Diplomasia

Umoja wa Ulaya waiwekea vikwazo serikali ya Ukraine

Kikao cha dharura cha mawaziri wa Ulaya, mjini Brussels. Huu anaetangulia hapa mbele ni waziri wa mambo ya nje wa Italia, Emma Bonino.
Kikao cha dharura cha mawaziri wa Ulaya, mjini Brussels. Huu anaetangulia hapa mbele ni waziri wa mambo ya nje wa Italia, Emma Bonino. AFP

Bunge nchini Ukraine limepiga kura ya kuwataka maofisa wa polisi wa kupambana na ghasia nchini Ukraine kuondoka katika ngome za wapinzani jijini Kiev. Juma hili polisi wamekuwa wakikabliana na waandamanaji machafuko ambayo yamesabisha vifo vya watu zaidi ya sabini wakiwemo maafisa wa usalama.

Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa Mambo ya nje wa umoja wa Ulaya wamekubaliana kuiwekea serikali ya Ukraine vikwazo.

Waandamanaji nchini humo wamekuwa wakiandamana tangu mwezi novemba mwaka uliopita baada ya serikali kukataa kutia saini mkataba wa biashara na Umoja huo na wameendelea kushinikiza ni sharti rais Viktor Yanukovich ajiuzulu.

Machafuko ya jana pekee yamesabaisha watu 60 kupoteza maisha, kulingana na taarifa iliyotolewa na upinzani, huku juhudi za mawaziri watatu wa mambo ya nje wa Ulaya za kutaka kusuluhisha pande mbili zikiwa imeendelea usiku kucha tangu jana alhamisi hadi leo ijumaa.

Kwa upande wake Washington imepaza sauti, na kutishia kuchukua vikwazo dhidi ya “viongozi wa ngazi ya juu wa Ukraine ambao wanahusika katika machafuko yanayoendelea nchini humo”, ujumbe ambao umewasilishwa moja kwa moja na makamu rais Joe Biden kwa rais wa Ukraine Viktor Ianoukovitch, huku waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ametoa wito wa kusitisha machafuko, na mauaji “kwa watu wasiyokua na hatia”.

“Zaidi ya waandamanaji 60 wameuawa kwa kupigwa risase kwa siku ya jana, amesema mmoja wa viongozi wa hospitali zinazomilikiwa na upinzani, Sviatoslav Khanenko. Wanahabari wa AFP wameshuhudia kwa siku ya jana miili ya watu 25 waliyo uawa kwa risase.

Idadi ya watu waliyouawa imefikia 75 tangu jumanne, wizara ya afya imefahamisha jana jioni.