Ikulu ya Mogadishu nchini Somalia imerejea kwenye umiliki wa vikosi vya Serikali baada ya shambulizi la Al shabab

Eneo la Ikulu ya Somalia ambalo kundi la wanamgambo la Alshabab lilishambulia
Eneo la Ikulu ya Somalia ambalo kundi la wanamgambo la Alshabab lilishambulia

Ikulu ya Mogadishu nchini Somalia imerejea kwenye umiliki wa vikosi vya Serikali, kufuatia mashambulizi ya makomandoo wa Al-Shabab waliojaribu kuvamia ikulu ya rais.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa Somalia, Abdikarim Hussein Guled amewaambia wanahabari mjini Mogadishu kuwa baada ya saa kadhaa za makabiliano kati ya vikosi vya Serikali na wanamgambo hao wamefanikiwa kuwafurusha na kuilinda Ikulu ya rais Hassan Sheikh Mohamud.

Wanamgambo wa Al-Shabab walitumia magari kujitoa muhanga na kurusha maroketi kwenye Ikulu lakini hawakufanikiwa kuingia ndani, kufuatia ulinzi mkali uliopo kwenye Ikulu ya Mogadishu.

Umoja wa Mataifa UN umesema kuwa rais, Hassan Sheikh Mohamud hakujeruhiwa kwenye shambulio hilo, ambalo ni kubwa zaidi kuwahi kufanywa na wanamgambo hao kulenga Ikulu ya Mogadishu.