UKRAINE-Maandamano

Waandamanaji wapiga kambi mji kiev Licha ya rais Yanukovych kutangaza kufikia makubaliano na upinzani

WWaandamanaji wapiga kambi mji kiev Licha ya  rais Yanukovych kutangaza kufikia makubaliano na upinzani
WWaandamanaji wapiga kambi mji kiev Licha ya rais Yanukovych kutangaza kufikia makubaliano na upinzani REUTERS/Olga Yakimovich

Maelfu ya waandamanaji wameendelea kusalia mjini Kiev licha ya mpango uliokusudiwa kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Ukraine ambao watu kadhaa wamepoteza maisha.

Matangazo ya kibiashara

Mpango uliosainiwa ijumaa kati ya raisi Viktor Yanukovych na upinzani unatamka kuundwa kwa serikali ya muungano na kufanyika kwa uchaguzi wa raisi.

Hata hivyo inabainishwa kuwa watu wengi hususan waandamanaji bado hawana imani na raisi Yanukovych.

Maraisi wa Marekani na Urusi wamekubaliana kuwa mpango huo unapaswa kutekelezwa haraka.

Ikulu ya Marekani imebainisha kuwa Urusi imetaka kuhusika katika mchakato wa utekelezwaji.