SYRIA-UN-Mazungumzo

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lapitisha bila kupingwa azimio la ufikishwaji wa huduma za kibinadamu nchini Syria

Wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakiwa mkutanoni
Wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakiwa mkutanoni RFI

Baraza la Usalama la umoja wa mataifa limepitisha bila kupingwa azimio linaloomba kuruhusiwa kwa misafara ya misaada ya kibinadamu kufika na kutoa huduma katika eneo lenye vita nchini Syria, lakini wanadiplomasia tayari wameonyesha shaka juu ya ufanisi wake.

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Urusi ambayo ni Mshirika mkubwa wa Syria ikiungwa mkono na China, imepinga maazimio matatu katika kipindi kilichopita China, maazimio yaliyolenga kuishinikiza serikali ya Damascus tangu kuanza kwa mgogoro nchini humo mwezi Machi mwaka 2011,huku wastani wa nusu ya wasyria wote wakiwa wanasubiri msaada wa haraka.

Lakini serikali za Moscow na Beijing ambazo ni wanachama wawili kati ya wanachama watano wa kudumu wa Baraza la Usalama, hazikufanya hivyo wakati huu, jambo linalotuma ujumbe wenye nguvu kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad, ambaye utawala wake unashutumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki katika kujaribu kung'ang'ania madarakani.

Azimio hilo ambalo pia linakosoa hatua ya ndege za serikali kuangusha mapipa ya mabomu, liliandaliwa na nchi za Australia, Jordan na Luxembourg naliliungwa mkono na Uingereza, Ufaransa na Marekani, wanachama wengine wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.