VENEZUELA-Maandamano

Rais Nicolas Maduro aanza mazungumzo na upinzani kujaribu kutuliza maandamano

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, mei 19 nchini Brezil.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, mei 19 nchini Brezil. Ueslei Marcelino/Reuters

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro amesisitiza utayari wake wa kufanya mazungumzo na taasisi mbalimbali nchini humo wakiwemo wapinzani kujaribu kupata suluhu ya kutuliza maandamano ya vurugu ambaye yamekuwa mtihani wake wa kwanza toka aingie madarakani. Rais Maduro amefahamisha kwamba amewaalika wakuu wa mikoa, wakiwemo wale wa upinzani, kukutana leo kwa mzungumzo.

Matangazo ya kibiashara

Akiwahutubia wafuasi wake nje ya Ikulu ya Caracas, rais Maduri amewataka upinzani, taasisi za kidini na zisizo za kiserikali kukutana nae siku ya Jumatano ya jumahili kufanya mazungumzo ili kumaliza maandamano yanyoendelea kuigawa nchi hiyo.

Wananchi pamoja na wanafunzi, wanaandamana nchi kupinga Serikali ya Maduro kwa kile wanachodai toka ameingia madarakani kumekuwa na hali ngumu ambapo wananchi wanakosa hata huduma muhimu huku bei za vitu zikipanda.

Rais Maduro amesema maandamano hayo ni mpango wa kutaka kuipindua Serikali yake iliyochaguliwa kuhalali.

Mapema leo asubuhi, mamia ya wafuasi wa utawala, wengi wao wakiwa ni watu wazima, wameandamana katika mji mkuu wa Venezuela, Caracas, wakionesha kwamba wanamuunga mkono rais Maduro. Rais Maduro alikabiliwa na maandamano ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika kipindi cha majuma matatu yaliyopita, ambapo watu kumi walipoteza maisha.

Vijana, sitisheni maandamano yenu, hii ni nchi ya amani, tunataka liwe na amani ya kudumu”, Cristina Marcos, mwenye umri wa miaka 60, ameambia vyombo vya habari, wakati wa maandamano hayo.

Makabiliano makali yalitokea juzi jumamosi jioni kati ya waandamanaji wanaopinga utawala wa rais Maduro na kikosi cha usalama, na kusababisha watu 25 kujeruhiwa.