SYRIA-Diplomasia

Serikali ya Syria iko tayari kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kutoa misaada maeneo yanayokumbwa na vita

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wakiidhinisha azimio namba 2139
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, wakiidhinisha azimio namba 2139 RFI

Utawala wa Damascus nchini Syria, umesema kuwa uko tayari kuendelea kushirikiana na Umoja wa Mataifa UN katika kutoa misaada kwenye maeneo yenye vita, iwapo tu Umoja huo utaheshimu uhuru wa taifa hilo, huku wanaharakati wa haki za binadamu na mashirika ya kutoa misaada masikitiko yao kuona hakuna hatua ziliyochukuliwa iwapo serikali haitotekeleza iliyojikubalisha.

Matangazo ya kibiashara

Azimio hilo liidhinishwa jumamosi iliyopita na baraza la Umoja wa Mataifa,Urusi ambaye ni mshirika wa karibu wa wa utawala wa Bachara al-assad, imekubali kushiriki uchaguzi na kuidhinisha azimio hilo, ambapo awali ilitishia kulipinga kwa kutumia kura yake ya turufu.

Serikali ya rais Bashar al-Asad inasema kuwa iko tayari kutekeleza azimio lililopitishwa na baraza la usalama mwishoni juma kutaka kuongezwa zaidi kwa operesehni za misaada kwenye miji inayokabiliwa na vitra nchini humo ili kunusuru maisha ya raia wasio na hatia.

Kupitishwa kwa azimio hili kuliungwa mkono pia na nchi za Urusi na China ambazo awali zilipinga azimio kama hilo kwa kile ilichodai kuwa liliegemea upande mmoja wa waasi.

Azimio namba 2139 linatoa agizo kwa mashirika ya misaada kuruhusiwa kupita na kuingia kwenye maeneo yenye vita bila kubugudhiwa na vikosi vya Serikali wala vile vya waasi.

Machafuko nchini Syria yamesababisha watu 140,000 kupoteza maisha katika kipindi cha miezi mitatu, huku mamia kwa mamilioni ya raia wakiyahama makaazi yao, kulingana na taarifa iliyotolewa na shirika linalotetea haki za binadamu nchini Syria (OSDH).

Hayo yakijiri, saudia arabia inadaiwa kua iko katika mazungumzo na Pakistan kwa kuwapatishia silaha waasi wa Syria ili waweze kukabiliana na mashambulizi ya anga na aridhini yanayoendeshwa na jeshi la Syria, kulingana na duru ziliyo karibu na faili hii.