MISRI-Siasa

Baraza la mawaziri nchini Misri lajiuzulu

Waziri mkuu wa Misri Hazem el-Beblawi, akiwa  Abou Dhabi, oktoba 27 mwaka 2013.
Waziri mkuu wa Misri Hazem el-Beblawi, akiwa Abou Dhabi, oktoba 27 mwaka 2013. REUTERS/Ben Job/Files

Baraza lote la mawaziri lililoteuliwa kuunda serikali na utawala wa kijeshi nchini Misri, limetangaza kujiuzulu hapo jana, hatua inayokuja ikiwa umebaki takriban mwezi mmoja na nusu kabla nchi hiyo ifanye uchaguzi wake mkuu. Kujiuzulu kwa baraza hilo la mawaziri kumeonekana kuwashtua walio wengi huku wananchi wakibaki na maswali ni kitu gani kilichopelekea kujiuzulu kwa waziri mkuu Hazem al-Beblawi.

Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa hatua hiyo inalenga kumpa nafasi Jenerali Fattah al-Sisi kuwania nafasi ya urais kwenye uchaguzi ujao pamoja na jeshi kuunda serikali ya muda kuelekea uchaguzi mkuu.

Wapo pia wanaoona kuwa kuna mgawanyiko hata ndani ya baraza lenyewe la mawaziri.

Waziri mkuu wa Misri, Beblawi jana ametangaza kujiuzulu, baada ya kuteuliwa kushikilia wadhifa huo tangu alipotimliwa rais aliyechaguliwa Mohamed Morsi, julai 3 mwaka 2013.

Tangu wa kati huo, mamia kwa maelfu ya wafuasi wa Morsi walianadamana, na baadhi yao waliuawa na vikosi vya usalama, vikibaini kwamba maadamano hayo yalikua kinyume cha sheria.

Hayo ya kijiri, kiongozi wa majeshi, ambaye alimng'oa madarakani rais Morsi, Abdel Fattah al-Sissi, atajitangaza, kulingana na dura ziliyo karibu naye, kugombea kwenye kiti cha urais.

Sissi, ili ashikiliye, wadhifa huo, inampaswa ajiuzulu serikalini na jeshini, au astaafu jeshini.

Uchaguzi nchini Misri unatazamiwa kufanyika mwaka huu.