SYRIA-Mapigano

Jeshi nchini Syria ladai kuuwa waasi zaidi ya mia moja

Mapigano makali yaripotiwa karibu na mji wa Damascus, nchini Syria.
Mapigano makali yaripotiwa karibu na mji wa Damascus, nchini Syria. Reuters

Zaidi ya waasi kumi wameuawa na jeshi la Syria katika shambulizi la kuvizia, wakati waasi hao walipokua wakijaribu kuingia katika mji wanaoshikilia karibu na mji wa Damascus, taarifa hii imetolewa na televisheni ya serikali pamoja na shirika moja la kihisani la nchini Syria.

Matangazo ya kibiashara

“Kupitia upelelezi wetu na ujuzi wetu wa kuvizia amabo ulikua ameandaliwa vizuri, jeshi letu limefanikisha kuua waasi wa kundi la Al-Nosra katika miji ya Ghouta na Damascus, ambao wengi wao ni raia wa kigeni, na tumefaulu kukamata silaha zao”, zimeendelea kufahamisha taarifa hizo ziliyotolewa kupitia televisheni ya taifa.

Eneo la Ghouta mashariki linalopatikana mashariki ya mji mkuu wa Syria, Damascus, ni eneo muhimu kwa waasi dhidi ya utawala wa Bachar al-Assad, ambao umekua ukidai kwamaba waasi hao ni “magaidi”.

Jimbo hilo lilishuhudiwa mauaji ya mamia ya watu katika mwaka wa 2013 kutokana na shambulizi liliyotekelezwa kwa kutumia silaha za kemikali, shambulizi ambalo lilipelekea mataifa ya magharibi kutishia kufanya mashambulizi dhidi ya utawala wa Bachar al-Assad.

Kundi la Al-Nosra,linalowakilisha rasmi kundi la Al-Qaïda, limekua likishirikiana na makundi mengine ya waasi katika mapigano ya kijeshi katika kipindi cha miaka mitatu sasa dhidi ya utawala wa Assad.

Duru za usalama zimefahamisha kwamba kundi linaloundwa na raia kutoka Jordan na Saudia Arabia, wamepenya na kuingia kwenye aridhi ya Syria, na baadaye yakatokeya mapigano ambayo yamepelekea waasi 156 kuuawa na wengine kumi kushikiliwa.