VENEZUELA-Mazungumzo ya kitaifa

Mazungumzo ya kitaifa yaanza nchini Venezuela : Upinzani wakataa kushiriki

Rais wa Venezuela anatazamiwa kuanzisha leo mazungumzo ya kitaifa na wadau wote, lakini viongozi wakuu wa upinzani wamekataa kushiriki mazungumzo hayo. Rais Nicolas Maduro anakabiliwa na maandamano dhidi ya utawala wake kwa kipindi cha majuma matatu sasa, maandamano ambayo yamesababisha machafuko.

Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akiwahutubia wafuasi wake mbele ya Ikulu, Miraflores, mjini Caracas, februari 25 mwaka 2014.
Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro akiwahutubia wafuasi wake mbele ya Ikulu, Miraflores, mjini Caracas, februari 25 mwaka 2014. AFP-Francisco Batista
Matangazo ya kibiashara

Ajenda ya mazungumzo hayo ya “kusaka amani”, haijawekwa wazi na rais Maduro, ambaye ni mrithi wa Hugo Chavez.

Henrique Capriles, alieshindwa na Maduro katika uchaguzi wa urais uliyofanyika mwezi wa aprili, amesema kwamba hatoshiriki mazungumzo hayo, akibaini kwamba ni upuuzi mtupu na uongo wa rais Maduro.

Lakini rais Maduro amebaini kwamba katika mazungumzo hayo watafikiya mkataba maridhawa.

Mazungumzo hayo yanafanyika wakati, wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Venezuela wameitisha maandamano jumamosi, baada ya majuma matatu kukishuhudiwa maanamano yaliyozua vurugu wakipinga utawala wa rais Nicolas Maduro.

Marekani ilielezea hivi karibuni wasiwasi wake juu ya hali inayojiri nchini Venezuela. Rais Maduro, amefahamisha kwamba atamfukuza balozi wa Marekani nchini mwake.

Mataifa hayo mawili yamekua hayana kwa kipindi kirefu mabalozi wanaoyawakilisha katika taifa mojawapo.

Maandamano hayo yanaendelea, wakati serikali ilianza kukutana tangu jumamosi na wadau wote, ili kuanzisaha mazungumzo ya kitaifa.

Awali upinzani nchini humo ulikataa kushiriki kwenye mazungumzo yaliyoitishwa na rais Maduro hii leo wakisisitiza kwanza kuachiliwa kwa viongozi wa kisiasa wanaoshikiliwa na vyombo vya usalama.

Rais Maduro ameema jana kwamba kuna mkono wa mataifa ya magharibi kutaka kuipindua Serikali yake kupitia maandamano hayo yanayoendelea.

Mapema juma hili katika miji mingine, kama Valencia, mji wa tatu kwa ukubwa nchini Venezuela, kulitokea machafuko yaliyosababishwa na makabiliano kati ya waandamanaji na polisi, ambao walilazimika kufyatua risase za plastiki na mabomu ya kutoa machozi dhidi ya vijana waliyokua waliweka viziwizi kwenye barabara inayoelekea mjini.

Nicolas Maduro, mrithi wa kisiasa wa Hugo Chavez (katika miaka ya 1999-2013), ambaye alifariki kutokana na maradhi ya saratani machi 5 mwaka 2013, amekua akinyooshea kidole cha lawama Marekani kwamba imekua ikiunga mkono upinzani ili uendeleye na machafuko hayo.

Maduro amesema maadui wa taifa hilo, wameamua kuzua fujo ili waipinduwe serikali yake.