JAMHURI YA AFRIKA YA KATI-Diplomasia

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati apongeza uamzi wa bunge la Ufaransa

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza
Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza Issouf Sanogo/AFP

Rais wa mpito wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Catherine Samba-Panza, ameridhishwa na raia wa Ufaransa, ambao wamekubali kuendelea kuinga mkono nchi yake kwa juhudi za kusaka amani na usalama kwa raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, msemaji wake ameelezea jana AFP, baada ya Ufaransa kuchukua jana uamzi wa kuongeza muda wa operesheni “sangaris” kwa kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa waliyo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Matangazo ya kibiashara

“Rais ameelezea furaha yake kwa Ufaransa na (rais wa Ufaransa), François Hollande kwa juhudi wanazozifanya ilio nchi ya Jamhuri ya Afrika kati ipate amani na usalama”, amesema msemaji wa rais, Clément-Anicet Guiyama-Massogo.

Duru ziliyokaribu na ikulu zinafahamisha kwamba rais Samba-Panza atalihutubia leo jumatano taifa, kufuatia hatua ya bunge la Ufaransa ya kuidhinisha pendekezo liliyotolewa na serikali ya Ufaransa ya kuongezea kikosi cha wanajeshi wa Ufaransa kusalia Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Wabunge wa Ufaransa wameruhusu kuongezewa muda wa miezi minne operesheni ya kijeshi “Sangaris” nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, licha ya waziri mkuu, Jean-Marc Ayrault, kuonesha matatizo kadhaa yanayowakabili wanajeshi hao wa Ufaransa nchini jamhuri ya Afrika ya Kati.

Katika mauzugumzo ya hivi karibuni na AFP, rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, aliomba Ufaransa “kutoitupilia” Jamhuri ya Afrika ya Kati.

“Huu si muda wa kuitupilia Jamhuri ya Afriaka ya kati. Nina imani kwamaba uamzi uttakaochukuliwa hivi karibuni na bunge la Ufaransa utakua ni sambamba na matakwa ya wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambao wanaendelea kuwa na matumaini makubwa kwa msaada unaotolewa na jumuiya ya kimataifa, hususan Ufaransa”, amesema rais Samba-Panza.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesabaishwa na hali ya kutovumiliana kati ya wakristo na waislamu, baada ya kundi la waasi wa Séléka, ambao wengi wao ni waislamu, kuuteka mji wa Bangui machi mwaka 2013, na kuanza mauaji dhidi ya wakristo.

Siku chache baadaye kundi la wakristo la anti-balaka liliendesha mauaji dhidi ya raia wasiyokua na hatia kutoka jamii ya waislamu, na kudai kwamba wamekua wakijilipiza kisase dhidi ya mauaji ya watu kutoka jamii ya wakristo yaliyokua yakitekelezwa na waasi wa Séléka