SUDANI KUSINI-Usalama

Wagonjwa wauawa wakiwa wamelazwa hopitalini nchini Sudan Kusini

Wafanyakazi wa shirika la madaktari wasiyo na mipaka wa kihudumia wagonjwa katika hospitali moja ya mji wa Jonglei, nchini Sudan Kusini.
Wafanyakazi wa shirika la madaktari wasiyo na mipaka wa kihudumia wagonjwa katika hospitali moja ya mji wa Jonglei, nchini Sudan Kusini. RFI

Watu wasiyojulikana, ambao wanadhaniwa kuwa wapiganaji wa makundi yanayozozana nchini Sudan Kusini, wametekeleza mauaji dhidi ya wagonjwa katika hospitali mbalimbali na kupora dawa na vifaa vingine vinavyotumiwa kwa kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa, limethibitisha shirika la madaktari wasiyo na mipaka (MSF).

Matangazo ya kibiashara

Shirika hilo limebaini kwamba mamia kwa malfu ya raia nchini Sudan Kusini kwa sasa hawapati huduma za matibabu.

Katika tangazo llake, shirika la madaktari wasiyo na mipaka, wameonya dhidi ya ongezeko la mashambulizi dhidi ya wagonjwa na uporaji wa vifaa vinavyotumiwa kwa huduma za matibabu kwa wagonjwa.

Sudan Kusini imekumbwa na mgogoro tangu desemba 15 mwaka jana kati ya jeshi linalounga mkono serikali na kundi la wanajeshi waliyoasi wanaomuunga mkono aliye kua makamu wa rais, Riek Machar.

Mamia ya raia wamepoteza maisha kutokana na machafuko hayo, huku watu 900,000 wakiwa wameyahama makaazi yao.

MSF imelani visa vya mauaji dhidi ya wagonjwa, uchomaji moto wa dawa, na uporaji wa vifaa vinavyotumiwa kwa huduma za matibabu kwa wagonjwa.

“Mashambulizi hayo yanaonesha ukosefu wa nidhamu kwa afya ya binadamu, na ukukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa kuwakosesha wagonjwa kupata huduma wanazohitaji, amesema Raphaël Gorgeu”, mkuu wa MSF nchini Sudan Kusini.

Mgogoro wa Sudan Kusini unatokana na kupigania madaraka kati ya rais wa nchi hio, Salva Kiir na makamu wake wa zamani,ambaye alifutwa kazi mwezi julai mwaka jana, Riek Machar.

Rais Salva Kiir anamtuhumu Machar kupanga njama za kuipindua serikali yake.
Riek Machar anakanusha tuhuma hizo dhidi yake na kudai kwamba Salva Kiir amekua hataki watu wngine ambao watagombea urais kupitia chama tawala.

Shirika la madaktari wasiyo na mipaka, linabaini kwamba watu 300,000 kwa sasa hawapati huduma yoyote ya matibabu, na hakuna dawa zinazopatikana katika hospitali.