UKRAINE-Siasa

Rais wa mpito wa Ukraine aonya nchi ya Urusi kuingilia kijeshi nchi yake

Rais wa mpito wa Ukraine, Olexandre Tourtchinov.
Rais wa mpito wa Ukraine, Olexandre Tourtchinov. AFP/SERGEI SUPINSKY

Rais wa mpito wa Ukraine ameitahadharisha meli ya Urusi ilioko katika bahari Nyeusi kwenye mpaka na Ukraine kutothubutu kuingila kijeshi nchi yake, hayo ni wakati watu wenye silaha wenye mafungamano na Urusi wamevamia mapema leo asubuhi majengo ya serikali katika mji wa Crimea, chini Ukraine. 

Matangazo ya kibiashara

“Ninawaambia viongozi wa kijeshi wa kikosi kiloko kewnye bahari nyeusi: wanajeshi wote wanapaswa kusalia katika maeneo yaliyopangwa na mkataba. Mwanajeshi wowote atakaetoka katika eneo lake na kuelekea eneo lingine, itaonekana kuwa ni uchokozi”, amesema rais wakati alipokua akilihutubia bunge.

Mji wa Crimea, ni eneo la Ukraine ambamo raia wanazungumza lugha ya kirusi, umekua ukitoa hifadhi kwa meli ya kijeshi ya Urusi kwenye bahari Nyeusi.
Zaidi ya watu kumi wamevamia mapema leo asubuhi majengo ya serikali na bunge katika mji wa Crimea, ambapo wameshusha bendera.

Waziri wa mambo ya ndani wa Ukraine, Arsen Avakov, amesema kwamba ameomba polisi na kikosi maalumu kuwa tayari kukabiliana na mashambulizi yoyote.

Crimea, yenye raia wengi wanaoongea kirusi, ni jimbo la Ukraine amabo linaweza kwa wakati wowote kupinga viongozi wapya walioko madarakani mjini Kiev, baada ya rais Viktor Ianoukovitch kutimuliwa. Awali jimbo hili lilikua chini ya mamlaka ya Urusi, kabla ya kujiunga na Ukraine katika mwaka 1954.