Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-

Chama cha Frelimo nchini Msumbiji chamteuwa Filipe Nyussi kugombea kiti cha Uraisi

Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Fillipe Nyussi kuwakilisha chama cha FRELIMO katika mbio za uraisi nchini humo.
Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Fillipe Nyussi kuwakilisha chama cha FRELIMO katika mbio za uraisi nchini humo.
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Chama tawala nchini Msumbiji Frelimo kimemteuwa waziri wa ulinzi Filipe Nyussi kuwa mgombea wa kiti cha uraisi kupitia chama hicho jana jioni, uamuzi ambao huenda ukashuhudia raisi wa sasa Amando Guebuza akiendelea kuwa na ushawishi hata mara baada ya kuondoka madarakani kufuatia kura za mwezi Octoba.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa chama cha Frelimo Damiao Jose aliiambia AFP kuwa Filipe Nyusi alishinda asilimia 68 ya kura zote baada ya mizunguko miwili ya kupiga kura.

Wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho walishangilia kwa furaha kufuatia ushindi wa Nyusi na kumpongeza waziri huyo mkutano huo wa kisiasa kutamatika usiku wa manane huko Matola nje kidogo ya mji mkuu Maputo.

Kiongozi huyo mteule Filipe Nyusi alitoa pongezi kwa Frelimo akimaanisha harakati za zamani za kudai uhuru zilizosimamiwa na chama hicho Frelimo.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.