Pata taarifa kuu
Afrika Kusini-Rwanda-Uchunguzi

Serikali ya Kigali yawafukuza wanadiplomasia wa Afrika Kusini nchini Rwanda kujibu hatuwa kama hiyo ya serikali ya Afrika Kusini

Raisi Wa Rwanda Paul Kagame
Raisi Wa Rwanda Paul Kagame rfi
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Serikali ya Rwanda imechukuwa hatuwa ya kuwafukuza wanadiplomasia wa Afrika Kusini Jijini Kigali baada ya serikali ya Johanesbourg kuchukuwa hatuwa kama hiyo ya kuwafukuza wanadiplomasia watatu wa Rwanda katika ubalozi wa Rwanda nchini humo baada ya kutuhumiwa kuhusika katika shambulio dhidi ya makaazi ya kiongozi wa zamani wa Rwanda  aliyepewa hifadhi nchini humo Kayumba Nyamwasa.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka jijini Kigali nchini Rwanda zimearifu kuwa serikali ya nchi hiyo imewafukuza wanadiplomasia sita wa Afrika Kusini jiji Kigali nchini hapo baada ya serikali ya rais Jacob Zuma kuamuru kufukuzwa kwa wanadiplomasia watatu wa Rwanda  nchini Afrika ya kusini.

Afrika Kusini inawatuhumu wanadiplomasia hao wa Rwnda kujihusisha na vitendo vya Ujasusi nchini Afrika Kusini ambapo hivi karibuni watu wenye silaha walivamia makaazi ya Faustin Kayumba Nyamwasa aliyewahi kuwa kiongozi wa majeshi ya Rwanda kabla ya kikimbilia nchini Afrika Kusini.

Hata hivyo wakati wa shambulio hilo mkosoajii wa rais Paul  Kagame, Kayumba Nyamwasa hakuwepo nyumbani kwake

Jenerali Kayumba Nyamwasa ameponea chupuchupu majaribio mawili ya kutaka kumuua ambapo mnamo mwaka 2010 alipigwa risasi na kujeruhiwa, tukio ambalo Rwanda ilikanusha kuhusika.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.