Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-RWANDA-Diplomasia

Pritoria yathibitisha kuwa na vithibitisho dhidi ya wanadiplomasia kutoka Rwanda waliyofukuzwa

Jeff Radebe, waziri wa sheria wa Afrika Kusini, hapa ni katika mwaka 2009, anathibitisha kuwa na vithibitisho dhidi ya wanadiplomasia kutoka Rwanda waliyofukuzwa..
Jeff Radebe, waziri wa sheria wa Afrika Kusini, hapa ni katika mwaka 2009, anathibitisha kuwa na vithibitisho dhidi ya wanadiplomasia kutoka Rwanda waliyofukuzwa.. PICHA : AFP / ALEXANDER JOE
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Serikali ya Afrika Kusini imeionya nchi ya Rwanda na kudai kuwa ardhi yake haitatumika kama uwanja wa vita kati yake na mataifa ya magharibi siku chache baada ya taifa hilo kuwafurusha maafisa watatu wa ubalozi wake wanaotuhumiwa kupanga njama za kuwashambulia wanasiasa wa Rwanda wanaoishi nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na wanahabari mjini Pretoria, waziri wa sheria, Jeff Radebe amesema kuwa kamwe nchi yake haitokubali kuona taifa lolote lile duniani likitumia ardhi yake kufanya shughuli zozote ambazo zinahatarisha usalama wa nchi na raia wake.

“Jambo la kwanza ni kwamba uhusiano wa kidiplomasia baina ya Afrika kusini na Rwanda ni mzuri na utaendelea kuwepo. Hata hivyo, serikali ya Afrika kusini imeamua kuwafukuza maafisa wa Rwanda na Burundi kwa sababu wamekiuka ibara ya 41 ya mkataba wa Viena na ibara ya 9 ya makubaliano kuhusu hadhi ya kidiplomasia. Haya ni matokeo ya kujihusisha na majaribio ya kuuwa mmoja wao anayeishi nchini Afrika kusini. Sisi ni nchi ya kideemokrasia ya kikatiba, na mtu yoyote yule au kundi la watu watakaokiuka haki za binadamu atakumbana na mkono wa sheria”, amesema Radebe.

Katika hatua nyingine Serikali ya rwanda imejibu mapigo kupitia waziri wake wa mambo ya Kigeni, Louise Mushikiwabo ambaye kupitia mtandao wa Twitter ameitaka Afrika kusini kuacha kuwapa hifadhi wahaini wa nchi hiyo ama sivyo ikubali gharama ya kile kinachotokea.

Maafisa watatu wa ubalozi wa Rwanda akiwemo na mmoja kutoka nchini Burundi walifukuzwa juma liliyopita nchini Afrika Kusini, hatua ambayo ilichukuliwa na serikali ya nchi hiyo, ikiwatuhumu kuhusika katika mashambulizi ya kuhatarisha usalama wa wakimbizi wa Rwanda na Burundi wanaomba hifadhi nchini Afrika Kusini.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.