Ukraine-mzozo

Kura ya maoni leo Crimea kuamua kujiunga na Urusi au Kiev

Urusi imeimarisha majeshi yake huko Crimea wakati huu zoezi la kura ya maoni lichukua nafasi
Urusi imeimarisha majeshi yake huko Crimea wakati huu zoezi la kura ya maoni lichukua nafasi REUTERS/Vasily Fedosenko

Wananchi katika eneo la Crimea nchini Ukraine wanapiga kura ya maoni itakayoamua kujiunga na Urusi au kubaki na serikali ya kiev ambayo inaungwa mkono na mataifa ya magharibi yanayoona uchaguzi huo ni haramu.

Matangazo ya kibiashara

Majeshi ya Urusi yamedhibiti katika eneo hilo lenye watu wengi wenye asili ya Urusi wakati huu kukiwa na baadhi ya wapigakura wakitazamiwa kupigia kura kubaki na serikali ya Ukraine,huku wengine wanaounga mkono Ukraine wakipanga kugomea zoezi hilo.
Urusi mapema ilipigia kura ya turufu kupinga rasimu ya azimio la Umoja wa mataifa kukosoa kura hizo isipokuwa mwanachama wa Baraza hilo ndiye anaruhusiwa kufanya hivyo.

Hati hiyo ambayo iliandaliwa na marekani iliungwa mkono na mataifa 13 wanachama wa baraza la usalama huku China ikionekana kama Urusi.

Hapo jana Watu wawili waliuawa nchini Ukraine katika jiji la mashariki la Kharkiv kufutia ghasia kuzuka kati ya wanaharakati wa ukraine na wanaounga mkono Urusi.