UKRIANE-CRIMEA-UChaguzi

Raia wa kisiwa cha Crimea wapiga kura ya kujiunga na Urusi

Raia wa mji wa Simféropol, katika kisiwa cha Crimea, wakiwa foleni wakisubiri wapewe kadi ya uchaguzi, 16 machi.
Raia wa mji wa Simféropol, katika kisiwa cha Crimea, wakiwa foleni wakisubiri wapewe kadi ya uchaguzi, 16 machi. VIKTOR DRACHEV/AFP

Wananchi katika eneo la Crimea nchini Ukraine wamepiga kura ya maoni kuamua kujiunga na Urusi kwa kura asilimia 96.6. Matokeo hayo ni ya mwisho, kulingana taarifa iliyotolewa mapema leo asubuhi na waziri mkuu anaeunga ushirikiano na Urusi, Serguiï Axionov, katika anuani yake ya mtandao wa kijamii wa twitter.

Matangazo ya kibiashara

“Matokeo ya mwisho ya kura ya moni ni asilimia 96,6 kwa kura ya ndio”, ameendika Axionov. Bunge la Crimea linatazamiwa kukutana ili kuidhinisha rasmi matokeo hayo ya kisiwa cha Crimea kujiunga na Urusi, huku kura hio ya maoni ikionekana kutotambuliwa na utawala wa Kiev na mataifa ya magharibi.

Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono nchi ya Urusi, wameandamana katika mji wa Donetsk mashariki mwa Ukraine kuonesha kuunga mkono haki ya Crimea kujiunga na Urusi na kusisitiza kutoa maoni yao wenyewe katika suala hilo.

Waziri mkuu wa Ukraine Arseniy Yatsenyuk ameomba kupelekwa haraka kwa waangalizi wa kigeni kutoka Shirika la usalama na ushirikiano wa Ulaya OSCE, katika eneo la Mashariki na Kusini mwa nchi hiyo wakati huu Crimea ikitishia kujitenga na kujiunga na Urusi.

Serikali mpya ya Ukraine na kiasi kikubwa cha Jumuiya ya Kimataifa isipokuwa Urusi wamesema hawata yatambua matokeo ya kura hiyo.