URUSI-UKRAINE

EU yaongeza vikwazo kwa Urusi

Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy
Rais wa Umoja wa Ulaya Herman Van Rompuy www.telegraph.co.uk

Umoja wa Ulaya umetangaza vikwazo zaidi kwa watu mashuhuri nchini Urusi kutokana na mzozo wa Ukraine na kuwawekea vikwazo vya kusafari watu wengine 12 kutika nchini Urusi na kuzuia mali yao barani Ulaya na pia kutangaza kuwa imesitisha mkutano kati ya Umoja huo na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Vikwazo vya Umoja wa Ukaya vinakuja saa chache baada ya rais wa Marekani Barrack Obama kutangaza vikwzo zaidi dhidi ya Urusi, kwa kuwanyima washirika wa karibu wa rais Vladimir Putin Viza za kwenda Marekani.

Moscow nayo imetnagza vikwazo vya kutosaforoi kwa wanasiasa kwa wanasiasa kadhaa wa serikali ya Marekani kwenda Moscow.

Haya yote yanatokana na kura ya maoni iliyopigwa katika jimbo la Crimea nchini Ukraine, na waakzi wa eneo hilo kukubali kujiunga na Urusi suala ambalo Mtaufa ya Magaribi yanasema inakwenda kinyume na sheria za Kimataifa.