UKRAINE-Siasa

Ukraine yasaini mkataba wa ushirikiano na Umoja wa Ulaya

Премьер-министр Украины Арсений Яценюк на пресс-конференции в Брюсселе 06/03/2014
Премьер-министр Украины Арсений Яценюк на пресс-конференции в Брюсселе 06/03/2014 REUTERS/Yves Herman

Waziri mkuu wa muda nchini Ukraine Arseniy Yatsenyuk ameithibitisha nchi yake kuwa upande wa mataifa ya Magharibi, kwa kusaini mkataba wa ushirikiano na viongozi wa Ulaya na kuiweka kando Urusi

Matangazo ya kibiashara

Rais wa umoja wa Ulaya Hermann Van Rompuy amesema kuwa Ishara hiyo ni alama ya umuhimu zilionao pande zote katika uhusiano huo, na kwamba muungano huo utaendelea zaidi ya hapo.

Umoja wa Ulaya ilikuwa ikiiunga mkono nchi ya Ukraine kwa nguvu zote , ambapo Van Rompuy ameahidi kuisaidia nchi hiyo kuinua uchumi wake ambao unatetereka.

Baada ya viongozi 28 wa mataifa yanayounda umoja huo wa Ulaya kusaini makubaliano hayo, waziri mkuu Yatsenyuk amesema kuwa ana uhakika kwamba kwa pamoja watafanikiwa kutimiza malengo.

Mkataba huo,ulioandaliwa kwa miaka, ulitupiliwa mbali ghafla na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Viktor Yanukovych mnamo mwezi Novemba na kusababisha maandamano yaliyomwondoa madarakani mwezi uliopita na kuchochea mzozo mbaya wa mataifa ya magharibi na mashariki tangu kumalizika kwa vita baridi.

Masharti ya kisiasa ya makubaliano ya ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Ukraine yatahusu maadili ya pamoja ya kidemokrasia, mahusiano bora ya kiuchumi, mageuzi ya mahakama na mambo mengine ya asasi za kiraia.