MAREKANI-UKRAINE-Diplomasia

Urusi yatazamiwa kuchukuliwa hatua ya kuondolewa katika kundi la mataifa tajiri duniani

Rais wa Marekani Barack Obama.
Rais wa Marekani Barack Obama. RFI

Rais wa Marekani Barack Obama amewasili leo asubuhi nchini Uholanzi kwa mazungumzo, ambamo mzozo wa Ukraine utapewa kipau mbele, na kuna hatari Urusi ichukuliwe hatua ya kuondolewa katika kundi la mataifa tajiri, kutokana na hatua uamzi wake wa kujisogezea kisiwa cha Crimea, baada ya viongozi na raia wa kisiwa hicho kuamua kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa mataifa 7 tajiri wanakutana leo jioni katika mji wa La Haye kwa jitihada za rais wa Marekani, Barack Obama, katika mkutano kuhusu usalama wa nuklia, wakti ambapo majeshi ya Urusi yaliteka mkesha wa kuamkia leo ngome mpya ya jeshi la Ukraine katika kisiwa cha Crimea.

Ngome ya Feodossia imetekwa baada ya vifaru na helikopta za kijeshi vya Urusi kuishambulia. Wanajeshi wa Ukraine wameondoka kwene ngome yao hio, wakiwa wamebebwa ndani ya malori.

Urusi umedhibiti kwa sasa kisiwa cha Crimea, ambacho Moscow inakichukuliya kama moja ya sehemu yake, baada ya viongozi na raia wa kisiwa hicho kujitenga na Ukraine na kujiunga na Urusi, na kupelekea mataifa ya magharibi kuangalia upya uhusiano wao na Kremlin, ambao haukua mzuri tangu mwishoni mwa vita baridi.

Wakati Moscowa ikiendelea kuongeza idadi ya wanajeshi wake kwenye mpaka na Ukraine, baadhi wana hofu kwamba, Vladmir Putin ana lengo la kudhibiti maeneo mengine ya Ukraine.

Mkutano huo kuhusu usalama wa nuklia uliyopangwa kufanyika leo na kesho mjini La Haye, utaangazia mzozo unaoendelea nchini Ukraine.

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergueï Lavrov na mwenziye wa Marekani John Kerry, kando ya mkutano huo, wanataraji kukutana kwa mazungumzo, amabapo inaaminika kwamba yatakua mazungumzo ya kina tangu ulipo zuka mzozo wa Ukraine.

Itakua ni mazungumzo yao ya kwanza tangu Washington ilipowachukuliya vikwazo vya kifedha dhidi ya viongozi waliyo karibu na Vladmir Putin kutokana na uamzi wa Urusi wa kukubali kujiunga na kisiwa cha Crimea kilichojitenga na Ukraine.